MATAIFA YA EAC LAZIMA YALINDE WATOTO

Padri Dakta Steven Chogo, Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii kutoka TEC, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa JOLIFA Frida Manga Wajumbe na Wakufunzi kutoka Prolife Tanzania pindi walipowasilisha maoni juu Muswada wa Kijinsia na Afya ya Uzazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa mwaka 2021 kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC. ( Picha ya Maktaba) 

.....................

Na Richard Mrusha

Uhai wa Binadamu ni kitu Kitakatifu, ambapo asili yake ni Mungu mwenyewe, hivyo Kila mmoja anaalikwa katika kulinda, kuutetea na kuudumisha kwa nguvu zote.

Mtandao wa Waandishi wa Habari za Uhai na Familia Tanzania( JOLIFA TZ) umekusudia kutoa semina kwa Waandishi wa habari, kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa katika maswala ya ulinzi na Kutetea Uhai.

Mratibu wa Mtandao huo kwa Tanzania Frida Manga alisema semina hizo zitasaidia Waandishi wa habari kutumia kalamu Zao vyema kuandika habari za kuwaasa Viongozi katika Ngazi zote na hasa wa Serikali ambao ni watunga sera wanawajibu wa kuhakikisha sera wanazotunga hazitaingilia ama kuharibu Uhai wa Binadamu bali kulinda.

Manga alisema kadri siku zinavyosonga mbele Uhai wa Binadamu unakuwa kwenye hatari kana kwamba MUNGU hakumuumba mtu kwa Sura na mfano wake na kwamba amemuumba ili amjue, ampende, amtumikie na mwisho afike kwake Mbinguni. 

Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), zinawajibu kulinda Uhai wa Binadamu tangu kutungwa Mimba Hadi kifo cha Kawaida,

Aliongeza kuwa Viongozi wa ( EAC) wanawajibu wa kueleza wazi na ikiwezekana kuwa ajenda yao wanaposimama majukwaani kuzungumza na Wananchi juu ya athari za Ndoa za Utotoni, Matumzi ya Vithibiti Mimba na ukatili wowote unaolenga kuharibu Uhai wa Binadamu.

Ukatili dhidi ya watoto una athari za maisha yote kwa afya na ustawi wao. 

Uhai wa Binadamu ni kitu Kitakatifu, ambapo asili yake ni Mungu mwenyewe, hivyo kila mmoja anaalikwa katika kulinda, kuutetea na kuudumisha kwa nguvu zote.

Katika hili, Viongozi katika Ngazi zote na hasa wa Serikali ambao ni watunga sera wanawajibu wa kuhakikisha sera wanazotunga hazitaingilia ama kuharibu Uhai wa Binadamu bali kulinda.

Alisema Kuzuia urushaji Matangazo kwenye Vyombo vya habari yanayochochea wasichana kutumia vidhibiti mimba kwani Uwepo wa Matangazo hayo ni sehemu ya uhamasishaji wa Ngono kwa Watoto.

Viongozi wa ( EAC) wanawajibu wa kueleza wazi na ikiwezekana kuwa ajenda yao wanaposimama majukwaani kuzungumza na Wananchi juu ya athari za Ndoa za Utotoni, Matumzi ya Vithibiti Mimba na ukatili wowote unaolenga kuharibu Uhai wa Binadamu.

Ukatili dhidi ya watoto una athari za maisha yote kwa afya na ustawi wao kwani ni vigumu sana kwa watoto kusahau mambo maovu au ya kinyama wanayotendewa na jamii wakiwemo watu wa karibu. 

Kwa upande wake Mtakatifu Yohane Paulo II (Papa)katika waraka wake, "Injili ya Uhai" anasema kuwa Injili ya Uhai ndiyo kiini cha mafundisho ya YESU,

Ni ujumbe ambao Kanisa huupokea siku hadi siku kwa moyo wa upendo, na ambao Kanisa halina budi kuuhubiri kiaminifu na kwa ujasiri kama "habari njema" kwa watu wa nyakati zote na tamaduni zote.

Akiendelea, Baba Mtakatifu anasema kuwa Injili hii ya Uhai ambayo Kanisa imeipokea kutoka kwa Bwana Yesu Kristo ina nguvu na uwezo wa kupenya ndani kabisa ya moyo wa kila mwanadamu.

Haijalishi awe mwamini au sivyo, kwani Injili hiyo ya Uhai siyo tu inakidhi kwa namna ya ajabu matarajio yote ya moyo bali pia inapita kabisa hata upeo wake.

 Kanisa linajiona kuwa limeitwa kuwahubiria watu wa nyakati zote "Injili" hii, ambayo ni chemchemi ya matumaini yasiyovunjika na furaha ya kweli kwa kila kizazi. 

Hii ni Injili ya upendo wa Mungu kwa mwanadamu, Injili kuhusu hadhi ya mwanadamu na Injili ya uhai ni wimbo mmoja usiogawanyika.
 

0/Post a Comment/Comments