MTEMVU AWASHUKIA CCM DAR WAACHE KUGAWANYIKA

 




 ..........................

Na Heri Shaaban (Ilala )

MWENYEKITI wa CCM Mkoa Dar es Salaam Abas Mtemvu, amewataka wana CCM Mkoa Dar es Salaam kushirikiana kujenga umoja ndani ya chama cha Mapinduzi CCM wakileta mpasuko ndani ya chama itagharimu Uchaguzi Mwaka 2024 /2025.

Mwenyekiti Abas Mtemvu aliyasema hayo Wilayani Ilala Kata ya Kivukoni wakati DIWANI wa Kivukoni Sharick Choughule akiwasilisha Taarifa ya utekekezaji wa Ilani .

"Nawashukuru Dar es Salaam kuleta mshikamano nimeshinda kwa kishindo Uchaguzi wa chama Mkoa tusigawanyike  tutashindwa kufanya vizuri Uchaguzi wa Mwaka 2024 Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025"alisema Mtemvu.

Mwenyekiti Mtemvu amewataka wana CCM Dar es Salaam warudishe Umoja Ili wende vizuri katika UCHAGUZI  .

Akizungumzia Uteuzi wa Uchaguzi mdogo wa Kata ya Majohe Wilayani Ilala  chama Cha Mapinduzi mapendekezo yaliopendekezwa Kata ya Majohe na CCM Wilaya Ilala CCM Mkoa wamepitisha hakuna mgombea yoyote atakaye katwa jina Mkoa Dar es Salaam katika chaguzi zote wataheshimu mapendekezo yao

Akizungumzia Utekelezaji wa Ilani amempongeza Diwani Sharick kwa Utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2021/ 2022 amewataka Madiwani wengine waige mfano  waandae Utekelezaji wa Ilani wamualike atafika katika Uwasilishaji  wa Ilani na kukagua Miradi kila Kata .

Akizungumzia ukosefu wa Ofisi ya  Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni alisema atazungumza na Naibu Spika wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania  Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ,anamtumia usiku na Mchana katika Utekelezaji wa Ilani kuakikisha Ofisi inapatikana Kivukoni .

Akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa HALMASHAURI ya Jiji Kwa Njia ya simu amemwagiza Ndani ya mwaka huu ofisi ipatikane Kivukoni .

0/Post a Comment/Comments