RAIS CHAKWERA WA MALAWI AWAPA KONGOLE LUGALO GOFU

 


Rais wa Malawi Mh Lazarus Chakwera (kulia ) Balozi wa Tanzania Malawi Mh Humphrey Polepole (Katikati ) na Mkuu wa Msafara wa Wachezaji kutoka Lugalo Gofu Meja Jenerali Ibrahim Mhona wakati wa kuzindua Mashindano ya Kuwaenzi Maveterani wa Vita.


 

 Rais wa Malawi Mh Lazarus Chakwera akipiga mpira wa gofu ikiwa ishara ya  kuzindua Mashindano ya Kuwaenzi Maveterani wa Vita Lilongwe Malawi

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


RAIS wa Malawi Mh Lazarus Chakwera ameishukuru Tanzania kupitia  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda  kwa ushirikiano inaouonyesha  kwa nchi hiyo na jeshi lake kupitia michezo ikiwemo mchezo wa Gofu.

Rais Chakwera ameyazungumza hayo Leo Novemba 05, wakati wa sherehe za ufungaji wa mashindano ya  gofu ya kuwaenzi na kuwachangia maveterani wa vita yaliyofanyika katika Uwanja wa Gofu wa Lilongwe nchini Malawi.

“ Ninanawashuru Ndugu zetu kutoka Tanzania  hakuna nchi ambayo haipati Changamoto za kiuchumi na hakuna Nchi ambayo haipambani kutatua shinda za wananchi wake na mahitaji yao lakini kikubwa ni kusaidiana na Kuchangiana kufanikisha hilo ."

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi wa Malawi Jenerali Vicent Nundwe amesema ni heshma kubwa kwa jeshi lao kupata ugeni huo ambao umezidi kuongeza ushirikiano.

“ Najua mmesafiri kutoka Mbali kuja Malawi hii ni heshima kubwa kwetu tunawashukuru sana kwa kuacha shughuli zenu na kuja kutuunga mkono katika Mashindano haya.”

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mh Humphrey Polepole amsema kama Ubalozi wanamshukuru Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda kwa kuruhusu utekelezwaji wa Diplomasia kupita Michezo.

""Imekua siku nzuri kwa shindano hili kutokana na  timu yetu kutoka jeshi kutoka Lugalo Gofu kufanya vizuri katika shindano la kuwaenzi na kuwachangia maveterani wa vita."

Polepole ameongeza kuwa ushirikiano wa nchi ya Tanzania na Malawi katika shindano hilo sio tu kufanikisha kufanya harambee ya Kuchangia meterani waliopigana Vita nchini Malawi bali pia inakuza uchumi kutokana na taasisi na makampuni mbalimbali kuonyesha dhamira ya kudhamini shinda hilo kupitia mchezo wa gofu.

"Huu ni mwendelezo wa kidiplomasia ya kisiasa lakini pia kimichezo na upande mwengine kiuchumi kutokana na taasisi nyingi kushiriki katika Shindalo hili."

Naye Mkuu wa Msafara wa timu ya golf ya  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo  Meja Jenerali Ibrahim Mhona ameeleza kuwa safari imekuwa na manufaa makubwa  kwa Majeshi ya nchi zote mbili.

"Kimsingi tumefanikiwa kufanikisha Shindalo hili na zaidi tunashukuru ushirikiano wa Rais wa Malawi  maneno yake yanaonyesha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi ya Tanzania na Malawi. "

Aidha Mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amefafanua zaidi kuwa kwa Upande wa Klabu Baada ya Mashindano klabu sasa inajipanga kwa Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara.

Mbali na wachezaji wa Golf Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania liliwakilishwa pia na vikundi vya sanaa kutoka Mwenge ambavyo vilitumbuiza kwa pamoja na vikundi vya sanaa kutoka Malawi.


MWISHO.

0/Post a Comment/Comments