SERIKALI KUIMARISHA MFUMO WA USIMAMIZI NA UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI BLUEPRINT.

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dar es salaam.

Naibu katibu mkuu wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara Ally Gugu akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam.

Picha ya pamoja wahariri wa vyombo vya habari pamoja na waziri wa uwekezaji viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji (aliyeketi katikati)


.....................

Na: Issa Mohamed –Dar es salaam.

Email: issamohamed765@gmail.com

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji amesema serikali itaendelea kuondoa vikwazo kwa wawekezaji kuanzia ngazi ya halmashahuri ili kurahisisha uwekezaji nchini na kuongeza tija katika pato la Taifa.

Dkt Kijaji ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam  katika mkutano uliowaleta pamoja wahariri wa vyombo vya, waandishi wa habari pamoja na watengeneza vipindi vya uwekezaji lengo ni kujadili mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji -MKUMBI.

amesema tayari serikali imeanzisha dirisha la pamoja la kuwahudumia wawekezaji ambapo taasisi zote za serikali zinazohusika na wawekezaji zimekutanishwa pamoja ili kupunguza usumbufu kwa wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza nchini.

‘’Kwa wale wanaokwamishwa kule halmashahuri tumetengeza idara kwenye sekretarieti za mikoa na shughuli zote zinatafinyika katika mfumo kwa kungiza documentary zake, wale waliokuwa wanakwamisha kwa maslahi yao binafsi tumefunga huo mlango’’ amebainisha Dkt Kijaji

Amesema katika zao la tumbaku kumekuwepo na mikakati madhubuti ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kufikia malengo yaliyowekwa huku wakulima wa tumbaku wakielimishwa kufuata mbinu bora za kilimo ili wazalishe kwa tija.

Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara Ally Gugu amesema wizara hiyo imekusudia kuhamasisha wafanyabiashara ili kukuza biashara zao.

‘’Lengo la mkutano huu ni kupeana elimu zaidi kuhusu mpango wa serikali wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekeza pamoja kusisitiza taasisi zote kutoa huduma kwa weledi’’ Amesema Gugu.

Aidha katika kipindi cha mwaka 2017/18 hadi 2019/20 serikali imefuta au kupunguza jumla ya tozo, ada na adhabu 232 hali iliyosaidia kupunguza gharama hasa kwa wajasiriamali wadogo na wakati -SME's.


 

0/Post a Comment/Comments