SERIKALI YA TANZANIA KUJA NA MIKAKATI KATIKA SEKTA YA BAHARI.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Marry Maganga akizungumza Jijini Dar es salaam katika akifungua ya siku ya nne ya kikanda lengo ni kujadili matumizi bora ya sekta ya Bahari.

Wadau mbalimbali walihodhuria warsha ya siku nne iliyoanza leo Novemba 28, 2022

Viongozi na wadau mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja akiwemo Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Marry Maganga (Katikati kwa walioketi).


.......................

Na: Issa Mohamed –Dar es salaam.

Email: issahmohamedtz@gmail.com

Katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Marry Maganga amesema serikali inatarajia kuweka mpango wa matumizi bora ya bahari ikiwa ni pamoja na kuweka mipaka kwa ajili ya sekta ya uvuvi, mafuta na usafirishaji.

Maganga ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya kikanda yenye lengo la kujadili matumizi bora ya sekta ya bahari na kukutanisha nchi takribani 10 huku Tanzania ikiwa ni mwenyeji wa mafunzo hayo.

Amesema hatua hiyo itaondoa muingiliano wa shughuli za kibinadam na kugawa maeneo yatakayotumika na shughuli husika na kuchangia Pato la Taifa kupitia uchumi wa buluu.

‘’Bahari ina rasilimali nyingi ni vizuri kukawa na utaratibu wa sisi binadam kutumia rasilimali hiyo kutokana na baadhi yetu hufaidika kupitia uvuvi, kwahiyo lazima zitumike kwa utaratibu ili kuwa endelevu’’ Amesema Bi Maganga.

Kwa upande wake Meneja wa Tafiti za mazingira kutoka baraza la Taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira –NEMC, Rose Mtui amesema mkutano huo utasaidia kujenga uwelewa hasa katika kipindi hiki Tanzania inaelekea uchumi wa buluu.

‘’Mkutano huu ni muhimu sana kwasababu naharini kuna kazi nyingi kama vile mafuta, uvuvi ma chumvi kwahiyo tusipopanga maeneo vizuri tutapata shida tutakapoingia uchumi wa buluu’’ Amesema Bi Mtui.

Naye Mhadhiri na mkuu wa idara ya sayansi afua na teknolojia ya uvuvi –Chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt Siyajari Pamba amesema kupitia mkutano huo watahakikisha wanapata takwimu kutoka kwa wataalamu wa mataifa mengine ili kuwa na mkakati wa pamoja.

Tafiti kutoka umoja wa Mataifa –UN uliowasilishwa juni 28 mwaka huu umebaini kuwa idadi ya watu waishio Pwani huchangia uchumi wa Dunia takribani dola trilioni 1.5 huku uhakikishaji wa mfumo wa ikolojia ya bahari utasaidi kukuza maisha ya wananchi

 

0/Post a Comment/Comments