SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA –NCH KUZINDUA SERA YA UBIA NOVEMBA 16 2022.

Meneja habari na uhusiano kutoka shirika la nyumba la Taifa -NHC Muungano Saguya (mwenye tai) akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaamWaandishi wa habari wakifatilia mazungumzo ya Meneja habari na uhusiano kutoka NHC Muungano Saguya

.....................

Na Issa Mohamed.

Jumla ya miradi 111 yenye thamani ya shilingi bilioni 300 imetekelezwa na shirika la nyumba la Taifa –NHC huku miradi 81 kati ya hiyo imekamilika kwa kugharimu shilingi bilioni 240 na miradi 30 yenye thamani ya shilingi bilioni 60 inaendelea kukamilishwa.

Utekelezaji wa miradi hiyo imetokana na  maboresho yaliyofanywa na shirika hilo kwa mwaka huu iliyotokana na sera ya ubia iliyoanzishwa mwaka 1993 na kufanyiwa maboresho kadhaa kulingana na wakati husika.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja habari na uhusiano kutoka shirika la nyumba la Taifa –NHC, Muungano Saguya ikiwa ni muelekeo wa uzinduzi wa sera ya ubia ya shirika hilo unaotarajiwa kufanyika novemba 16 Jijini Dar es salaam.

‘’Hii sera ikienda kuzinduliwa italeta tija kwa Taifa kwa kuongeza fursa za ajira, makazi na mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa kutokana na shughuli za biashara kuwa nyingi’’ Amebainisha Saguya

Katika hatua nyingine Saguya amesema uzinduzi wa sera ya ubia umezingatia maslahi ya wabia, shirika la nyumba la Taifa –NHC na Taifa kwa ujumla huku washiriki zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya nchi wamethibitisha kushiriki.

‘’Kwahiyo tukasema shirika ili kuweza kukidhi kiu hii ya wawekezaji ambao wamejitokeza kuwekeza mitaji yao hapa nchini Tanzania tumeona tusogeze mbele ili kutoa fursa kwa wawekezaji hawa kuhudhuria mkutano huo’’ Amesema Saguya

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.

0/Post a Comment/Comments