TBS YATOA UFAFANUZI KUHUSU UKAGUZI WA BIDHAA MBALIMBALI


Mkaguzi wa Shirika la Viwango Tanzania katika kitengo cha Ukaguzi wa bidhaa zinazoingia na kutoka nje ya nchi Andalalisye Asanga Mwakyone akieleza utendaji kazi wa Kitengo hicho kufuatia ziara ambayo imefanywa na wanahabari Katika Shirika Hilo.

Afisa Mkuu wa Usalama wa chakula TBS Colleta Sarimbo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
........................
NA MUSSA KHALID

Shirika la Viwango Tanzania –TBS limewataka waingizaji wote wa bidhaa nchini pindi wanapofika eneo mzigo unapoingia Bandari kavu au uwanja wa ndege kuhakikisha bidhaa zao zinahakikiwa kabla ya kuruhusiwa kuingia ili kufanyiwa uchunguzi kabla ya kuzisambaza.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkaguzi wa Shirika la Viwango Tanzania katika kitengo cha Ukaguzi wa bidhaa zinazoingia na kutoka nje ya nchi Andalalisye Asanga Mwakyone kufuatia ziara ambayo imefanywa na wanahabari katika Shirika Hilo.

Mwakyone amesema kuwa lengo la kufanya ukaguzi wa bidhaa kabla ya kuwasili ni ili kurahisisha utoaji wa mizigo bandarini na kuchochea biashara katika ukaguzi usiohusisha maabara mzigo ulipoingia.

"TBS baadhi ya bidhaa huzihakiki baada ya kuwasili Nchini huweza kutolewa Bandarini huku ikisubiri uchunguzi wa kimaabara yaani kibali cha masharti ambacho hakimruhusu mteja kusambaza na kuingiza sokoni bidhaa yake mpaka pale uchunguzi wa kimaabara utakapokuwa umekamilika" amesema Mwakyone

Amesema kuwa Shirika la Viwango Tanzania lina kampuni tano zinazofanya ukaguzi katika maeneo ya uzalishaji mkubwa wa bidhaa zinazoingizwa nchini ikiwa ni pamoja na CCIC Intertek , Bureau Veritas, SGS pamoja na TUV walioanza shughuli za ukaguzi mapema Agosti mwaka huu

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Usalama wa chakula TBS Colleta Sarimbo amesema wamekuwa wakisajili bidhaa za chakula na vipodozi kwa kuangalia ubora wa bidhaa pamoja na maeneo watakayotumia kuhifadhi bidhaa zao.

Kuhusu ukaguzi wa Jengo amesema wanafanya ukaguzi kwenye eneo Hilo kama linakidhi viwango vya kuhifadhi bidhaa Hizo na wataandika taarifa na kisha atalipa gharama na kupata kibali chake Kwenye Mfumo.

Hata hivyo amesema mkakati wao ni kuhakikisha vipodozi vyote vinavyoingia nchini na kutumika na watanzania vinakuwa na ubora ili kutomdhuru mtumiaji.

0/Post a Comment/Comments