UVCCM KISUTU WATOA MSAADA PHOTOCOPY MASHINE



.....................

Na Heri Shaaban(CCM ILALA )

VIONGOZI wa Umoja wa Vijana Kata ya Kisutu wametoa msaada wa photokopy Mashine na mashine ya printer Ofisi ya Umoja wa Vijana Wilaya ya Ilala .

Msaada huo ulikabidhiwa  Makao Makuu ya Umoja wa Vijana CCM Wilayani Ilala.

Akikabidhi msaada huo Mjumbe wa  Mkutano mkuu wa  WIlaya kutokea UVCCM Kata ya Kisutu Tousif Bhojan alisema anamapenzi mema na chama Cha Mapinduzi msaada huo aliyokabidhi kwa ajili ya Jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Ilala .

Tumesaidia Jumuiya yetu ya Vijana Photopy Mashine na printer kwa ajili ya kujenga Jumuiya yetu chaguzi zimeisha za Wilaya Sasa kilichobaki kujenga chama cha Mapinduzi vijana ni nguvu ya Chama "BHOJAN

Bhojan alisema watashirikiama na Jumuiya ya Umoja wa  vijana UVCCM katika kutatua changamoto mbalimbali .


Mwenyekiti wa  umoja  wa  vijana UVCCM Wilaya Ilala Juma Mizungu alimpokea msaada huo na kushukuru kwa ajili ya KUJENGA Jumuiya ya Vijana pale walipotoa Mwenyezi Mungu aweze kuwazidishia .

Mwenyekiti Juma Mizungu alisema Umoja wa Vijana wameshibisha watu wachache wenye moyo kama huo wa kujitolea kujenga  chama Cha Mapinduzi CCM .

Mwisho


 

0/Post a Comment/Comments