WAHITIMU TAKRIBANI 489 WANATARAJIWA KUTUNUKIWA VYETI NA CHUO CHA KODI NCHINI NOVEMBA 25


Mkuu wa chuo cha kodi Profesa Isaya Jairo akizungumza Jijini Dar es salaam kuelekea mahafali ya 15 yanayotarajia kufanyika Novemba 25.

........................

Na: Issa Mohamed –Dar es salaam.

Email: issahmohamedtz@gmail.com

Mamlaka ya mapato nchini –TRA kupitia chuo cha kodi –ITA, kimekusudia kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo watumishi wa mamlaka hiyo ili kuwezesha ukusanyaji wa mapato na kuiwezesha serikali kutekeleza miradi yake.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam na mkuu wa chuo hicho Profesa Isaya Jairo wakati akitoa taarifa kuelekea mahafali ya kumi na tano ambapo jumla ya wahitimu 489 sawa na ongezeko la asilimia 25.1 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti vya stashahada, shahada na astashahada.

Amesema miongoni mwa mafanikio ya chuo hicho ni kuzalisha wataalamu watakaoendana na uhitaji wa soko la ajira ndani na nje ya nchi ili kuleta afua katika sekta ya fedha.

‘’Tunategemea kutoa elimu au mafunzo masafa lakini kwa kutumia teknolojia ya kisasa ukizingatia chuo cha kodi ni chuo pekee hapa nchini ukanda wa afrika mashiriki na kati na kusini mwa afrika ambacho kina ithibati ya kutoa mafunzo ya forodha na kodi’’ Amebainisha Prof, Jairo.

Akielezea kuhusu mahafali hayo Profesa Jairo amesema wahitimu 194 watatunukiwa cheti ch uwakala wa forodha, 36 watatunukiwa cheti cha usimamizi wa forodha na kodi.

‘’Ongezeko hili linatokana na juhudi za chuo na mamlaka ya mapato kutangaza chuo chake katika kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanakidhi viwango na pia yana akisi mahitaji ya soko’’ Amesema Prof Jairo.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo yatakayofana Novemba 25 ni waziri wa  fedha na mipango Mwigulu Nchemba huku –ITA kimeanza utekelezaji wa mpango mkuu wa tano kwa kutoa mafunzo kwa njia ya kidigitali baada ya mpango wa nne kukamilika.

0/Post a Comment/Comments