WAKAZI WA ILALA WATAKIWA KUJITOKEZA KUSHIRIKI KAMPENI YA KINGA TIBA YA MATENDE NA MABUSHA

 





Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na. Majid Abdulkarim, Dar es Salaam

Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala, Bi. Charangwa Selemani ametoa wito kwa wananchi kuhamasishana na kushiriki kimamilifu katika zoezi la kampeni ya ugawaji wa Kingatiba kuthibiti Ugonjwa wa matende na mabusha (Ngirimaji) litakalo chukua muda wa siku tano kuanzia 21 hadi 25 Novemba,2022.

Bi. Chalangwa ametoa wito huo leo wakati akifungua kikao kazi cha uhamasishaji kamati ya huduma za afya msingi kwa ajili ya zoezi la utoaji wa kinga tiba za ugonjwa wa matende na mabusha katika halmashauri za Temeke, Kinondoni, Dar es Salaam Jiji mkoani Dar es salaam.

Bi. Chalangwa ameeleza kuwa ugonjwa huu huwapata watu wa jinsia zote wanaume na wanawake hivyo ni budi kila mwananchi atakayefikiwa katika kaya yake kujitokeza kupata kinga tiba ili kuweza kuepuka maambukizi ya vimelea vya ugonjwa huu.

Naye Mganga mkuu wa Halmashauri ya Ilala, Dkt Elizabeth Nyema amebainisha makundi ambayo hayataweza kupatiwa kinga tiba ya ugonjwa wa mabusha na matende ni akina wanawake wajawazito, mama wanao nyonyesha, wagonjwa sana na Watoto walioko chini ya miaka mitano.

“Kinga tiba hii itatolewa kwa Watoto wenye Zaidi ya miaka mitano na kwa wale wanaohisi walisha tumia kinga tiba hii wanaruhusiwa kumeza kinga tiba hii hivyo ndo maana zoezi hili linakwenda nyumba kwa nyumba”, amesisitiza Dkt. Nyema

Kwa upande wake Afisa Elimu Shule za Msingi Halmashauri ya Ilala, Mwalimu Sipora Tenga amesema wako tayari kusimamia kikamilifu zoezi la ugawaji wa kinga tiba shuleni ili kuhakikisha zoezi linafanyikiwa kwa ufanisi mzuri.

MWISHO

0/Post a Comment/Comments