Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati akizindua Bodi Mpya ya tano ya ushauri ya Chuo cha Maji katika hafla ambayo imefanyika katika chuo hicho jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti mpya ya bodi hiyo,Dkt Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya tano ya ushauri ya Chuo cha Maji katika hafla ambayo imefanyika katika chuo hicho jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Cha Maji Dkt Adam Omari Karia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya tano ya ushauri ya Chuo cha Maji katika hafla ambayo imefanyika katika chuo hicho jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa bodi iliyomaliza muda wake,Dkt Sara Khamis, Nchimbi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya tano ya ushauri ya Chuo cha Maji katika hafla ambayo imefanyika katika chuo hicho jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo hicho ambao wamehudhuria wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya tano ya ushauri ya Chuo cha Maji katika hafla ambayo imefanyika katika chuo hicho jijini Dar es salaamWaziri wa Maji Jumaa Aweso akipatiwa zawadi ya picha yake iliyochorwa na mchoraji
.....................
NA MUSSA KHALID
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameitaka Bodi Mpya ya Chuo cha Maji kuhakikisha wanafanya utafiti wa kina ili watanzania wanapata huduma ya maji na kuondokana na changamoto.
Waziri Aweso ametoa kauli hiyo leo Jiji Dar es salaam wakati akizindua Bodi Mpya ya tano ya ushauri ya Chuo cha Maji ambapo amesema kuwa ni vyema Chuo hicho kikaonyesha jitihada za kujitofautisha na vyuo vingine ili mtu anapotoka hapo aonyeshe ubora zaidi katika eneo la maji.
Aidha Waziri Aweso amesema kuwa ameitaka bodi mpya ya ushauri ya chuo cha maji kuja na mikakati ya kukikuza chuo hicho ikiwa ni pamoja na kutumia fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini kwa kuhakikisha wanaanzisha vyanzo vya mapato .
Waziri Aweso amebainisha kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani pamoja na Wizara ya Maji wanaimani kubwa ya chuo hicho kwa kuzalisha wataalamu ambao watakwenda kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto za upatikanaji wa maji.
‘kuna miradi mingi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini ambayo inatumia fedha nyingi za Serikali lakini wanaopewa nafasi ya kusimamia miradi hiyo zikiwemo kamati za maji hazina watalaamu wa sekta ya maji’.amesema Aweso
Hata hivyo,Aweso,amekitaka chuo hicho kuandaa mafunzo ya kipindi kifupi kwa mafundi bomba wa mtaani ili waweze kupata ujuzi ambao utawarahishia kwenye kazi zao.
Awali Mkuu wa Chuo Cha Maji Dkt Adam Omari Karia amesema kuwa ili sekta hiyo iendelee kuwa endelevu watahakikisha wanafanikisha uboreshaji wa miradi mbalimbali sambamba na kuwapa ujuzi bora wanafunzi katika chuo hicho.
Naye Mwenyekiti mpya ya bodi hiyo,Dkt Rehema Nchimbi,ameomba ushirikiano kwa manajement ya chuo hicho Ili kuboresha utendaji wa chuo hicho.
Katika hatua nyingine waziri wa Maji Jumaa Aweso amewatunuku vyeti wahitimu 464 katika ngazi ya shahada, stashahada na astashahad mbalimbali za Chuo cha Maji na kuagiza wahitimu wa Chuo cha Maji ambao wamehitimu mafunzo yao ya kada mbalimbali katika chuo wapewe ajira ili wakasimamia miradi hiyo kote nchini
Post a Comment