WAZIRI MUHAGAMA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), mara baada ya Waziri huyo kuizindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Xavier Daudi na anaefuatia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Mhandisi Benedict Naomba


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict Ndomba akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya eGA kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka hiyo.

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx



Na  Richard Mrusha

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama  amezindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao itakayosaidia kupunguza tatizo la rushwa inayosababishwa na wananchi kukutana na watendaji mara kwa mara katika kupatiwa huduma.

Waziri Muhagama ameyasema  hayo Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya kwanza ya mamlaka ya serikali mtandaoni

Aidha Waziri Muhagama ameelekeza Bodi hiyo kusimamia vizuri majukumu yao ili kuondosha tatizo la rushwa kwasabu ya wananchi kukutana na watendaji mara kwa mara na kurahisha upatikanaji wa rushwa.

 Hata hivyo,Waziri Muhagama amesema juhudi zinazofanywa na Serikali ni kuhakikisha huduma zinafanyika kidigitali na kuchangia ukusanywaji mzuri mapato na kupelekea kuongezeka.

Vilevile,Waziri Jenista amesema Mamlaka hiyo imebeba siri kubwa ya matumizi ya mtandao na nia ya serikali ni kuajiri watu waaminifu na wazarendo watakaosimamia mifumo ya tehama.

Na kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya serikali mtandao,Mhandisi Benedict Benny amesema mamlaka hiyo utekelezaji wake  watasimamia jitihada za serikali mtandao katika ujenzi wa mifumo shirikishi na ya kisekta.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya wakuregenzi,Dkt Mussa Muhiddin,amesema watafanya kazi kwa ushirikiano kwa kufuata kanuni za za serikali mtandao.

0/Post a Comment/Comments