AJALI ZA BODABODA ZAPUNGUA,KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YATOA ELIMU HII KWAO.

 


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

IMEELEZWA kuwa Ajali za pikipiki nchini zimepungua toka Ajali 300 kwa mwaka 2021 mpaka kufikia ajali 279 kwa mwaka huu huku jitihada za makusudi za elimu za usalama Barabarani zikihitaji kupunguza Ajali hizo.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Mafunzo na Wakili wa Jeshi la Polisi, Deus Sokoni ,wakati wa kutoa mafunzo kwa waendesha boda jijini hapa ambapo mafunzo hayo yalifadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Limited

Aidha,Sokoni ametaja sababu iliyochangia kupunguza kwa ajali hizo kumetokana na utoaji elimu unaotolewa na jeshi la Polisi kupitia wadau mbalimbali ambapo elimu hizo zimeweza kuwajengea watu elewa kwa kuweza kuheshimu na kufuata sheria za usalama barabarani.

Sokoni amewataka Madereva hao hasa katika kipindi hiki cha sikukuu kuachana matumizi ya kupindukia ya kilevi wakati wanapoendesha vyombo vya moto ili kupunguza vitendo vya Ajali ambazo amedai baadhi yake zinasababishwa na ulevi.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Limited,Anitha Msangi, amesema kampuni inataoa mafunzo hayo ili kuweza kupunguza ajili za barabarani ambazo kwa kiasi kikubwa zinachangiwa na baadhi ya madereva kutozingatia sheria na kanuni .

Bi Msangi,Amesema kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi watahakikisha wateja wa kinywaji cha serengeni hawapati matatizo ndio maana wameona umuhimu wa kuja mafunzo hayo.

0/Post a Comment/Comments