Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Balozi wa Tanzania nchini Austria na mwakilishi wa Kudumu katika mashirika ya kimataifa Vienna, Mheshimiwa Balozi Celestine Joseph Mushy ameagwa katika Ibada ya Mazishi iliyofanyika nyumbani kwake Kibosho Road - Sambarai Moshi, Mkoani Kilimanjaro (Leo) Jumanne 20 Disemba 2022.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Stegomana Tax, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka waliungana na wawakilishi wa taasisi mbali mbali za kitaifa na kimataifa, ndugu na marafiki kutoa salam za pole na rambi rambi kwa familia ya Balozi Mushy.
Balozi Mushy alifariki dunia tarehe 15 Disemba 2022 kwa ajali ya gari wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga akiwa safarini kulekea Moshi, mkoani Kilimanjaro amezikwa kijijini kwake Kibosho.
Bwana ametoa, Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe.
Ameen.






Post a Comment