CHUO KIKUU MZUMBE CHAWAITA WAWEKEZAJI, NI KATIKA MAHAFALI YA 21


Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiwatunuku Shahada za Umahili wahitimu 240 katika fani mbalimbali, kwenye mahafali ya 21 ya chuo hicho yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.




Sehemu ya wahitimu wakitunukiwa Shahada za Umahili katika fani mbalimbali, kwenye mahafali ya 21 ya chuo hicho yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akikabidhi vyeti kwa watunukiwa waliofanya vizuri katika masomo yao katika fani mbalimbali, kwenye mahafali ya 21 ya chuo hicho yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akikabidhi vyeti kwa watunukiwa waliofanya vizuri katika masomo yao katika fani mbalimbali, kwenye mahafali ya 21 ya chuo hicho yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akikabidhi vyeti kwa watunukiwa waliofanya vizuri katika masomo yao katika fani mbalimbali, kwenye mahafali ya 21 ya chuo hicho yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Na Joachim Mushi, Dar

KAIMU Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Willium Mwegoha amewaalika wawekezaji mbalimbali kuchangamkia fursa za uwekezaji katika shughuli anuai za chuo kwa miradi ambayo inaweza kutekelezwa kwa ubia.

Profesa Mwegoha ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye Mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Mikutano Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Amesema Chuo hicho kina fursa za uwekezaji kwa ubia ikiwemo ujenzi wa hosteli za wanachuo, ujenzi wa maeneo ya biashara, michezo na burudani. Alieleza kuwa mfano kwa Chuo Kikuu Mzumbe Kituo cha Tegeta bado kinahitaji Mabweni kwa Wanachuo wa Kituo hicho hivyo kuwaalika wawekezaji walio tayari kushirikiana na chuo kujitokeza.

Aidha akifafanua zaidi alibainisha kuwa, Chuokina sera ya Uwekezaji ya mwaka 2020 ambayo inatoa fursa ya ubia na wawekezaji mbalimbali. 

Katika hafla ya mahafali hayo ya 21 Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amewatunuku Shahada za Umahili wahitimu 240 katika fani mbalimbali, ambapo idadi ya wahitimu wanawake inayoendelea kuongezeka kila mwaka ni 114 sawa na asilimia 47.5 huku wanaume wakiwa ni 126 sawa na asilimia 52.5.

Wanamahafali 89 wametunukiwa Shahada ya Umahili ya Biashara katika Menejementi ya Mashirika, wanamahafali 45 Shahada ya Umahili ya utawala wa Umma, Shahada ya umahiri ya Sayansi katika Menejiment Rasilimali watu wanamahafali 24, Shahada ya Umahiri ya Sayansi katika Uhasibu na Fedha 7 na Shahada ya umahiri ya Sayansi katika Menajimenti ya Ununuzi na Ugavi wakiwa 14.

Wengine ni Shahada ya umahiri ya Sayansi katika menejimenti ya Masoko 6, Shahada ya umahiri ya Biashara katika Menejimenti ya Mashirika, Watendaji Wakuu 13, Shahada ya umahiri ya Sayansi Katika Uchumi Tumizi na Biashara 14, Shahada ya Umahiri ya Utawala wa umma-Watendaji Wakuu 6 pamoja na Shahada ya Umahiri ya Uongozi na Manajimenti wahitimu 13.

Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Saida Yahya-Othman akizungumza na wanamahafali aliwataka kutumia elimu walioipata kutatua changamoto mbalimbali huko waendako.

"..Tukiwa tumemaliza Chuo, siyo tu vipi tutapata ajira, bali vipi tutadumisha heshima, ujuzi, uadilifu na ukombozi wa kifikra na kiuchumi, wetu wenyewe na wa jumuiya zetu. Elimu yetu inatakiwa iwe imetufungua siyo tu kiuchumi – ili tupate ajira, bali pia kisiasa – ili tujue haki zetu, na kijamii – ili tujue jamii na tamaduni zetu na vipi kuzilinda na kuzitetetea. Sehemu ya kufunuka akili ni kutambua yepi ya kuiga na yepi ya  kuyaepuka," alisisitiza Prof.  Yahya-Othman.


0/Post a Comment/Comments