WAKULIMA WA KAHAWA KARAGWE WAMSHUKURU RAIS DKT SAMIA HASSAN


 ..........................

Na Richard Mrusha Karagwe 

BAADHI ya wakulima wa kahawa wilayani Karagwe mkoani Kagera,wamemshukuru rais Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada kubwa za kuboresha kilimo ch zao hilo na kwamba sasa wameanza kunufaika kwa kupata bei zenye tija kwa uchumi wa kaya na familia kwa ujumla.

Pongezi za wananchi hao zimetolewa kwa nyakati tofauti na wakulima wa zao la kahawa wilayani humo,ambapo wamesema kwa msimu wa kilimo 2022/23 wamefanikiwa kuuza kahawa yao kwa njia ya mnada ambapo wamepata bei nzuri ya shilingi 2800 hadi 3,000 kwa kila kilo moja.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake muda mchache baada ya mwandishi wetu kutembelea shamba lake, James Fundulo, amemshukuru rais Dk. Samia kwa jitihada kubwa za kuongeza tija kwenye mazao ikiwemo kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima wa kahawa,na kwamba imemsaidia kujenga nyumba,kusomesha Watoto,na kununua gari.

Awali akizungumza na waandishi wa habari ofsini kwake, Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Mwl. Julieth Binyura amejivunia kuwa na wananchi wenye kutambua thamani ya kilimo huku akiyataja mazao yanayolimwa wilayani humo kuwa ni migomba,mahindi,maharage,viazi mvilingo pamoja na alzeti ambalo ni zao jipya kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Mwl. Binyula amesema miongoni mwa kata 23 za wilaya hiyo takribani aslimia 80 ya wananchi hao wanaishi kwa kutegemea kilimo na ufugaji,na kwamba kilimo cha biashara kimekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi hao.

Mbali na kumpongeza rais Dkt Samia,kwa agizo lake kuhakikisha wakulima wa kahawa wanauza kwa mfumo wa njia ya mnada, matokeo chanya yameanza kuonekana kwa wakulima wa wilaya hiyo ambapo kila mmoja amepata haki yake ndani ya siku mbili tu baada ya kuuza.

Amesema upande wa wananchi hao wanafuga kisasa na kwamba kupitia vyombo vya habari huwatangazia wananchi kwenda kujifunza kwa mwekezaji anayeitwa, Kahama Freshi, ambaye ni miongoni mwa wafugaji wanaofuga kitaalamu na wenye mafanikio makubwa.

Awali Kaimu Meneja wa Chama kikuu cha Ushirika (KDCU LTD), Domitian Kigunia alisema kuwa kuna vyama vya msingi 140 ambavyo vinawakulima wanachama zaidi ya 64,000 na majukumu yao makuu ni kuhakikisha vyama hivyo vinapata huduma stahiki ambapo chini yake kuna wakulima.

"Wajibu wa Chama chetu ni kuhakikisha vyama vya msingi vinapata masoko ya uhakika kwa ajili ya wakulima wao, lakini pia kutoa huduma zinazolenga kuleta tija katika uzalishaji kwa huduma ya ugani na kuwajengea uwezo wakulima hao ili kuzalisha kwa tija" alisema Kigunia na kuongeza.

“Tunaendelea na majukumu yetu kwa maana ya kuhakikisha mkulima anapata tija ya kutosha na kama chama kikuu chenye wanachama 140 tunahakikisha tunatoa huduma ambazo zina,muwezesha mkulima kuzalisha kwa tija ,huduma kama ambavyo kimsingi tunatekeleza nikuhakikisha tunakuwa na maofisa ugani na wanawahudumia wakulima na wanatoa elimu ya kilimo ili kuweza kuzalisha kwa tija na katika hilo chama kimeajili maafisa ugani 23na wapo vijiini na kazi yao na muda wao unatumika katika kuwajengea uwezo wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija”

0/Post a Comment/Comments