FCC YAWATAKA WAZALISHAJI BIDHAA NCHINI KUZINGATIA VIWANGO VYA UBORA WA BIDHAA ZAO


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania FCC William Erio wakati wa maonyesho ya saba ya bidhaa za viwanda nchini katika viwanja vya maonyesho Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam
............................ 

NA MUSSA KHALID

Tume ya Taifa ya Ushindani-FCC limewataka wazalishaji bidhaa mbalimbali nchini kuhakikisha bidhaa wanazozalisha zinakidhi viwango vya ubora ili kumlinda mlaji,kuvutia wawekezaji nchini na kuziwezesha bidhaa hizo kuingia katika soko la kimataifa.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania FCC William Erio wakati wa maonyesho ya saba ya bidhaa za viwanda nchini yanayofanyika katika viwanja vya maonyesho Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam na kusema ni vyema wazalishaji wajitahidi kuzingatia muonekano wa bidhaa ili kuvutia wateja.

Mkurugenzi huo amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wafanyabiashara kuwaeleza umuhimu wa kuzalisha bidhaa ambazo watu wengine hawatoweza kuziiga na kutengeneza za bandia zinazofanana na zao.

‘Tunawaeleza wafanyabiashara kuwa katika uzalishaji wao wafanye kazi kwa kushirikiana na FCC ili kuhakikisha kwamba bidhaa bandia haziingii sokoni na kuvuruga biashara zao’amesema Mkurugenzi Mkuu Erio

Aidha Erio amesema kuwa katika maonesho hayo lengo lao siokuuza tu bidhaa ndani ya nchi bali wafanyabiashara watumie fursa kutumia mawakala wanaosafirisha biadhaa nje ya nchi waweze kuuza bidhaa ili kupanua soko la mauzo yao na kuongeza kiwango cha biasharaa kinachouzwa.

Akizungumzia katika shughuli ya uzalishaji,amesema kuwa kilio kikubwa cha wawekezaji wa ndani imekuwa ni ukosefu wa mitaji hivyo amesema tume hiyo imekuwa ikishughulika masuala mitaji kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji.

Aidha Mkurugenzi mkuu wa FCC amesema tume hiyo imekuwa ikitoa elimu ya kufikia viwango vya ubora kwa wazalishaji wote wakiwemo watu wenye ulemavu kwa kufanya ziara mbalimbali, kuwapa semina na kuwahamasisha kushiriki katika maonesho mbalimbali nchini.

0/Post a Comment/Comments