FORUM CC NA ASASI ZINGINE ZA KIRAIA ZAJENGEANA UWEZO KUKABILIANA NA ATHARI MABADILIKO TABIA NCHI PAMOJA NA HAKI ZA MTOTO.


.............................

Taarifa na  salum Bitchuka

Asasi za Kiraia,taasisi za serikali na wadau wengine wametakiwa kuongeza uwajibikaji wao pamoja ili kuona ni kwa namna gani wanaweza kupunguza makali ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kizazi cha sasa ambacho ni watoto. 

Hayo yameelezwa Jijini Dar es Salaam na mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Mtandao wa mabadiliko ya tabia nchi Forum CC,  Sara Ngoi wakati wa mafunzo ya kujengeana uwezo kwa  asasi za kiraia kuona  namna ya kuhusisha masuala ya haki za watoto katika utekelezaji wao kwenye program zao za kila siku.

Sara amesema kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la athari za mabadiliko tabia nchi na athari hizo kwa namna nyingine zinahatarisha ufikwaji wa haki za mtoto  ikiwemo upatikanaji wa chakula,maji safi na salama, Afya pamoja na elimu.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki akiwemo Dickson  Strayton kutoka taasisi ya mtandao wa vijana  na mazingira Tanzania TAYEN na Afisa  mahusiano chama cha waandishi habari  za mazingira (JET) Tulinangwe Maloka  wamesema mafunzo hayo  yatawawezesha kutambua mbinu jumuishi za haki za bianadamu na programu za watoto katika suala zima la mabadiliko tabia nchi kwa kuhakikisha kwamba haki za mtoto na haki za bianadamu zinazingatiwa katika kukabiliana na athari chanya za mabadiliko tabia nchi.

Sanjari na mafunzo hayo Shirika la mtandao wa mabadiliko ya tabia nchi  Forum CC limezindua taarifa inayolenga kuelezea athari za mabadiliko  tabia nchi kwa mtoto na haki zake.

Mwisho.

0/Post a Comment/Comments