FORUM CC WATOA MAFUNZO KWA WATOTO KUHUSU ATHARI WAPATAZO WATOTO KUTOKANA NA MABADILIKO TABIA NCHI .





..............................

Salum Bitchuka

Imeelezwa kuwa kundi la watoto ndilo kundi linaloathirika zaidi kuliko makundi mengine katika mabadiliko  tabia nchi hapa nchini .

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Ushauri elekezi kutoka Shirika la Forum CC Baraka Machumu wakati wa mdahalo wa  kuangalia  madhara wanayopata watoto  yanayotokana  na mabadiliko tabia nchi.

Baraka amesema kati ya kundi la wazee na vijana kundi la watoto limekuwa likikosa  haki zao za msingi kutokana na mabadiliko tabia nchi  ikiwemo kukosekana elimu bora ,magonjwa na haki ya kucheza.

Kwa upande wao baadhi ya watoto walioshiriki mdahalo huo wamesema    wameweza kupata elimu ya kutosha kuhusu athari za mabadiliko tabia nchi na wao  wanakuwa mabalozi kuweza kutoa elimu hiyo kwa watoto wenzao.

Shirika la Forum CC wanatengeneza jukwaa la watoto kuweza kujifunza na kuelewa mabadiliko tabia nchi na namna gani watoto wanaweza kupaza sauti kuhusu mabadiliko tabia nchi.


 

0/Post a Comment/Comments