KATAMBI AZINDUA SOKO LA WAJASIRIAMALI, KITUO CHA URASIMISHAJI, UWEKEZAJI NA UENDELEZAJI BIASHARA, AKABIDHI GARI KWA VIJANA MANISPAA YA SHINYANGA

 


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu akikata utepe wakati akizindua Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu amezindua Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.


Hafla fupi ya uzinduzi wa Soko la Wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga, Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga na makabidhiano ya gari la Abiria (Coaster) imefanyika leo Jumapili Desemba 18,2022 na kuhudhuriwa na viongozi, wadau na wananchi mbalimbali wa Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Katambi Mhe. Katambi amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Mrisho Satura, Watumishi wa manispaa na Madiwani na viongozi wa Chama cha Mapinduzi ngazi zote wakiongozwa na Mwenyekiti na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna wanavyoshirikiana kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu  akizungumza wakati akizindua Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga.

"Kuna wale wanaopata kichefuchefu kuona Shinyanga tunajenga masoko, miundombinu, viongozi wanaelewana, kuona fedha zinazoletwa kwa ajili ya miradi mbalimbali. Kama una kichefuchefu na maendeleo lamba ndimu au hama Shinyanga",amesema Katambi.

“Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga ndugu yangu Dkt. Jomaary Satura anachapa kazi vizuri, Shinyanga sasa inabadilika. Tuna bahati mbaya Watu wenye uwezo mkubwa wakija Shinyanga wanapigwa sana majungu, wengine sasa wanataka ahamishwe. Hahami hapa, atahama hapa akiwa amepanda cheo maana uwezo wake ni mkubwa sana”,amesema Mhe. Katambi.
“Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga fanya kazi, umetumwa na Rais Samia, tuachane na majungu, Shinyanga sasa inapiga maendeleo. Achaneni na Ng’eng’eng’e tufanye maendeleo. Upende usipende lazima maendeleo yaje Shinyanga”,ameongeza Katambi.


Katambi ameeleza kuwa Maendeleo ya kweli yanahitaji watu wenye dhamira ya kweli kuleta maendeleo hivyo kuwaomba viongozi na wananchi kushikana pamoja ili kuibadilisha Shinyanga badala ya kuendeza majungu.

“Wanakuja watumishi wazuri Shinyanga lakini wanatishwa tishwa, kama wewe ni Mmafia basi mimi ni Mu Unguja na Pemba, tusitishane bwana, sisi tumetumwa kuleta maendeleo, acheni ng’eng’eng’e… Ng’eng’eng’e oyeeee”,amesema Katambi.

“Satura anafanya kazi nzuri, kiwango chake cha ufanya kazi ni kikubwa sana. Tunataka maendeleo kama hivi, hatutasikiliza majungu ya watu wenye kichefuchefu cha maendeleo. Shinyanga maendeleo ni lazima, Rais ameelekeza hivyo na Ilani imeelekeza hivyo”,ameeleza Katambi.


Akitoa taarifa kuhusu miradi hiyo mitatu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt, Jomaary Mrisho Satura amesema Ukarabati wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga umegharimu jumla ya shilingi Milioni 69 (69,939,400/=).

“Halmashauri ya Shinyanga ilipokea shilingi 32,000,000/= kwa ajili ya ukarabati wa kituo hiki. Aidha Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga iliahidi kuchangia shilingi Milioni 25 kwa ajili ya ukarabati wa One Stop Center hii kutoka katika mapato ya ndani ili kuhakikisha kuwa jengo linakuwa bora na la mfano. Hata hivyo hadi kufikia sasa halmashauri imechangia shilingi 37,939,400/= na kufanya fedha iliyotumika kufikia 69,939,400/=”,ameeleza Dkt. Satura.
Satura amezitaja huduma zitakazotolewa kwenye One Stop Center hiyo ni pamoja na kurasimisha biashara ndogo ndogo na za kati, kuratibu masuala ya uwekezaji kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya masuala ya biashara,kukuza mtaji wa mfanyabiashara kwa sababu taasisi za fedha zitatoa huduma katika kituo hicho, kumsaidia mfanyabiashara kupata masoko ya bidhaa na kuendeleza biashara za wajasiriamali wadogo na wa kati.

“Ukarabati wa umeshakamilika hivyo ni wakati muafaka wa kuweza kuzikabidhisha taasisi ambazo ni TCCIA, Benki,NSSF,SIDO,TRA, Manispaa ya Shinyanga (biashara,mapato,mazingira na utalii), uongozi wa machinga na wadau wengine kwa ajili ya kutoa huduma”,ameeleza  Dkt. Satura.

Kuhusu Jengo la Soko la Wajasiriamali maarufu jengo la Machinga Mjini Shinyanga, Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Shinyanga amesema ni sehemu ya mpango wa Halmashauri katika uboreshaji wa mazingira pamoja na kuvutia wateja wengi zaidi ili kuleta tija kwenye biashara zitakazokuwa zinafanyika kwenye eneo hilo.
Muonekano sehemu ya Soko la Wajasiriamali 'Machinga' Manispaa ya Shinyanga.

“Ujenzi wa soko hili ulioanza Mwezi Septemba 2022 na unatokana na hali mbaya ya miundombinu ya soko na wafanyabiashara 100 waliokuwa wakifanya biashara zao kwenye mazingira yasiyo rafiki hasa wakati wa mvua na jua. Ujenzi wa Jengo hili hadi kukamilika kwake umegharimu jumla ya shilingi 114,575,960/=”,amesema Dkt. Satura.

Akizungumzia kuhusu Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu kutoka kata ya Mjini katika Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Satura amesema vijana hao waliwekewa fedha ya mkopo kwenye akaunti yao na taratibu za kuagiza gari walizisimamia wenyewe.
Gari aina ya Nissan – Civilian

“Gari hili aina ya Nissan – Civilian kwa ajili ya kikundi cha vijana wabunifu Shinyanga linatokana na mkopo wa shilingi 60,000,000/= tulizowakopesha na watazirejesha kwa miaka mitatu. Kutokana na mkataba uliosainiwa kati ya halmashauri na kikundi hiki cha vijana ni kwamba litatumika kwa shughuli za biashara ya usafirishaji abiria ambapo kuanzia saa 12 hadi saa 2 asubuhi na kuanzia saa 10 hadi saa 12 jioni watawajibika kubeba wanafunzi kwa bei elekezi ya shilingi 200/300 ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi wapoenda shuleni na kurudi nyumbani na kuwaepusha na vitendo vya ukatili”,ameeleza Satura.

Hata hivyo amesema tangu mwaka wa fedha 2015-2016 hadi sasa, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imetoa mikopo ya jumla ya shilingi 1,565,730,419/= kwa vikundi 187 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu akizungumza wakati akizindua Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga leo Jumapili Desemba 18,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu akizungumza wakati akizindua Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt, Jomaary Mrisho Satura akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt, Jomaary Mrisho Satura akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga ndugu Ally Majeshi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anord Makombe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu akizungumza wakati akizindua Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu  na viongozi mbalimbali wakipiga makofi baada ya kukata utepe kuzindua Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu  na viongozi mbalimbali wakifurahia  kuzindua Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga
Maandishi kwenye Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga
Awali Afisa Biashara wa Manispaa ya Shinyanga Milembe akitoa taarifa ya ujenzi/ukarabati wa  Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akitoa taarifa kuhusu Gari aina ya Nissan – Civilian kwa ajili ya kikundi cha vijana wabunifu Shinyanga linalotokana na mkopo wa shilingi 60,000,000/= uliotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa Gari aina ya Nissan – Civilian kwa ajili ya kikundi cha vijana wabunifu Shinyanga linalotokana na mkopo wa shilingi 60,000,000/= uliotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu akizungumza wakati akikabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu akikata utepe wakati akikabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu na viongozi mbalimbali wakifurahia baada ya kukata utepe wakati akikabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu akiwa ndani ya Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu na viongozi mbalimbali  wakiwa wamepanda kwenye Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu akizungumza wakati akizindua Soko la Wajasiriamali 'Machinga' Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu akikata utepe wakati akizindua Soko la Wajasiriamali 'Machinga' Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu na viongozi wakifurahia baada ya kukata utepe wakati akizindua Soko la Wajasiriamali 'Machinga' Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya Jengo la Soko la Wajasiriamali 'Machinga' Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika Soko la Wajasiriamali 'Machinga' Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.
Viongozi na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu akiwaahidi kuwapa fursa mbalimbali Wasanii waliotoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.
MC Mzungu Mweusi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara (One Stop Center) Manispaa ya Shinyanga ,Soko la Wajasiriamali pamoja na kukabidhi Gari lililonunuliwa kutokana na Mkopo uliotolewa kwa kikundi cha Vijana Wabunifu katika Manispaa ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


0/Post a Comment/Comments