KIWANDA CHA MAGARI CHA GF VEHICLES ASSEMBLERS CHA SHINDA TUZO YA UBORA 2022/23

 

Kiwanda cha kwanza cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani kimeibuka mshindi wa kwanza kwa makampuni makubwa nchini wakati wa utoaji wa tuzo  za  Ubora wa Kitaifa wa makampuni bora kwa  Mwaka 2022\2023  zilizoandaliwa na shirika la viwango nchini TBS.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Kiwanda cha hicho, Ezra Mereng alisema  wanaipokea tuzo hiyo kwa furaha kutokana na kushiriki kwa mara ya kwanza na kuibuka kuwa washindi wa jumla katika kipengele cha makampuni makubwa.

Pia alisema tuzo hiyo inawahamasisha kuendelea kufanya kazi kwa bidii Zaidi ikiwezekana mwakani washinde tuzo za kimataifa za ubora wa bidhaa na itakayoweza kuzalisha magari na kuingia katika soko la ushindani kimataifa. Pia aliwashukuru wafanyakazi wenzake wakiongozwa na timu mzima ya wataalamu katika kutengeneza magari vitengo tofauti.

Nae mkurugenzi wa shirika la viwango nchini (TBS) Dkt. Athuman Ngenya aliwataka  GF kutoridhika na ushindi huo wa jumla nchini na wahakikishe wanashiriki mashindano  ya  nchi ya SADC katika ubora na viwango kwa makampuni ya jumuia hiyo.

Alisema kama wataibuka mshindi watapa tiketi ya moja kwa moja ya kushiriki  mashindano ya Ubora na viwango ya  jumuia ya SADC  na atakuwa anaiwakilisha Tanzania ambapo TBS watashirikiana na GF kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera ya Tanzania
Kwa kumalizia mkurugenzi Mtendaji wa  GF Vehicles Assemblers (GFA) Imrani Karmal  amewapongeza  wafanyakazi wake kwa umoja wao ndio chachu ya mafanikio ya wao kukidhi Ubora  katika uzalishaji wa magari bila wao wasingweweza kufanikiwa katika ushindi huo.

0/Post a Comment/Comments