MAHAFALI YA 39 CHUO CHA VETA SHINYANGA YAFANA

Wahitimu wa mafunzo ya Hatua ya Pili (Level II) katika fani mbalimbali wakiingia ukumbini kwa kucheza wakati wa Mahafali ya 39 ya Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mahafali ya 39 ya Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Desemba 2,2022 yamefanyika ambapo jumla ya wanafunzi 160 kati yao wanawake 40,wanaume 120 wamehitimu mafunzo ya Hatua ya Pili (Level II) katika fani mbalimbali.

Mahafali hayo yamefanyika katika Chuo cha VETA Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bw. Mhela Victor Mohamed.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Kaimu Mratibu wa Mafunzo katika chuo cha VETA Shinyanga, Jamary James Mayala amesema Chuo cha VETA Shinyanga kinatoa mafunzo ya kozi ndefu katika fani 10 na kozi fupi katika fani 27.

Amezitaja Fani Ndefu zinazotolewa katika Chuo cha VETA Shinyanga kuwa ni Fani ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa (Heavy Duty Equipment Mechanics), Fani ya Umeme wa Nyumbani (Electrical Installation) , Fani ya Useremala (Carpentry and Joinery), Fani ya Uchomeleaji na Uundaji vyuma (Welding and Metal Fabrication), Fani ya Ubunifu, Ushanaji na Teknolojia ya nguo (Designing, Sewing and Clothing Technology), Fani ya Bomba (Plumbing and Pipe Fitting), Fani ya Ujenzi (Masonry and Bricklaying), Fani ya Uhazili na Tehama (Secretarial and Computer Application), Fani ya Uendeshaji Mitambo (Plant Operation) na Fani ya Ukataji, Ung’arishaji na Uchoangaji wa Madini ya Vito (Gemstone cutting,polishing and carving).

Aidha amesema Chuo cha VETA Shinyanga pia kinatoa Mafunzo ya Muda mfupi katika fani 27 ambazo ni Fani ya magari, Fani ya umeme wa majumbani, Useremala, uungaji vyuma, ubunifu, ushonaji na teknolojia ya nguo,mabomba,ufundi uashi, uhazili na Tehama,uendeshaji mitambo,udereva, urembeshaji na mapambo, Tehama, umeme wa magari na utengenezaji wa batiki.

Fani zingine ni Madini (uchimbaji na ulipuaji miamba), upishi, usukaji wa motor, ufundi pikipiki, utengenezaji wa mitambo mikubwa,ufundi jokofu na viyoyozi, utengenezaji wa mitambo mikubwa,kudarizi, udereva wa bajaji na pikipiki,ufundi Kompyuta na ufundi mitambo mikubwa.

Aidha amesema mpaka sasa chuo cha VETA Shinyanga kina wanafunzi 382 wa kozi ndefu kati yao 255 ni wavulana na 127 ni wasichana na wanafunzi waliodahiliwa kuanzia Januari mpaka Disemba 2022 wa kozi fupi idadi yao ikiwa ni 1075 kati yao 858 ni wavulana na 277 ni wasichana.

Mbali na mafanikio lukuki waliyonayo bado Chuo cha VETA Shinyanga kilichoanzishwa mwaka 1989 kinakabiliwa na changamoto ya wanafunzi wa kutwa na watumishi kuchelewa kufika chuoni hasa nyakati za mvua kutokana na kutokuwepo kwa usafiri wa umama (Daladala), upungufu wa vyumba vya madarasa ya kutokana na mahitaji makubwa ya vijana kutaka kujifunza masomo ya ufundi stadi na baadhi ya wanafunzi wa kozi ndefu kuacha masomo kabla ya kozi kuisha kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele amewaomba wananchi kuchangamkia fursa ya mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho ili vijana wapate ujuzi na kujiinua kiuchumi kupitia fani zinazotolewa.

“Miundombinu yetu bado ni finyu, mabweni tuliyonayo yanachukua wanafunzi 170 tu. Tunakuomba mgeni rasmi kupitia jukwaa hili uhamasishe wafanyabiashara Manispaa ya Shinyanga waone fursa ya kujenga hosteli kwa ajili ya kupangisha ili kuongeza udahili wa wanafunzi wanaotoka nje ya Manispaa ya Shinyanga kwani chuo hiki kina eneo dogo pia ufinyu wa bajeti ya serikali katika kujenga miundombinu ya upanuzi wa chuo haraka”,amesema Mabelele.

“Tuna changamoto ya kutokuwa na mfumo wa majitaka katika Manispaa yetu ya Shinyanga hali inayopelekea kuongezeka kwa gharama za kusoma maji taka. Tunaomba jambo hili kama inawezekana tuingie mkataba na Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuondoa majitaka ili kupunguza gharama za kukodisha magari ya majitaka ambayo kwa sasa gharama ni kubwa sana”,ameongeza Mabelele.

Kwa upande wake mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bw. Mhela Victor Mohamed amesema halmashauri inatoa mikopo kwa vijana hivyo kuwashauri vijana hao kuchangamkia mikopo hiyo kwa kuunda vikundi ili kukabiliana na changamoto ya ajira na kwamba kuhusu suala la usafiri Manispaa itaanzisha usafiri wa umma hivi karibuni.

Hili suala la Public Transport halina muda mrefu, tuna mkurugenzi mwenye uwezo mkubwa hivyo tutatatua changamoto ya usafiri”,amesema Mohamed.

“Naomba wazazi mtambue kuwa Veta inaweza kuwafanya vijana kuwa na maisha ya kujitegemea wenyewe wakajipatia kipato. Hapa VETA kila ufundi upo wazazi leteni vijana wasome hapa ili wapate ujuzi na wazazi mliopo hapa muwe mabalozi wa kuiambia jamii kuleta watoto VETA ili watoto wapate ufundi wanaouhitaji”,amesema.
Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bw. Mhela Victor Mohamed akizungumza wakati wa Mahafali ya 39 ya Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Desemba 2,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bw. Mhela Victor Mohamed akizungumza wakati wa Mahafali ya 39 ya Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele  akizungumza wakati wa Mahafali ya 39 ya Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele akizungumza wakati wa Mahafali ya 39 ya Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Shinyanga 
Wahitimu wakisoma Risala wakati wa Mahafali ya 39 ya Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Mratibu wa Mafunzo katika chuo cha VETA Shinyanga, Jamary James Mayala akitoa taarifa ya mafunzo wakati wa Mahafali ya 39 ya Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Shinyanga
Awali mwakilishi wa Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA, Tajiri Molel akizungumza wakati wa Mahafali ya 39 ya Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Shinyanga
Wahitimu wa mafunzo ya Hatua ya Pili (Level II) katika fani mbalimbali wakiingia ukumbini kwa kucheza wakati wa Mahafali ya 39 ya Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Shinyanga
Wahitimu wa mafunzo ya Hatua ya Pili (Level II) katika fani mbalimbali wakiwa wamekaa
Vijana wa Kambi ya Nyani wakitoa burudani kwenye Mahafali ya 39 ya Chuo cha VETA Mkoa wa Shinyanga
Vijana wa Skauti wakikaanga mayai juu ya kichwa cha binadamu kwenye Mahafali ya 39 ya Chuo cha VETA Mkoa wa Shinyanga
Wahitimu wa mafunzo ya Hatua ya Pili (Level II) katika fani mbalimbali wakiwa wamekaa
Vijana wakitoa burudani kwenye Mahafali ya 39 ya Chuo cha VETA Mkoa wa Shinyanga
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya 39 ya Chuo cha VETA Mkoa wa Shinyanga
Onesho la ubunifu wa Begi linaloweza kutumika kama kitanda cha mtoto likiendelea kwenye Mahafali ya 39 ya Chuo cha VETA Mkoa wa Shinyanga
Wahitimu wa mafunzo ya Hatua ya Pili (Level II) katika fani mbalimbali wakiwa wamekaa
Burudani ya Igizo ikiendelea kwenye Mahafali ya 39 ya Chuo cha VETA Mkoa wa Shinyanga
Wahitimu wa mafunzo ya Hatua ya Pili (Level II) katika fani mbalimbali wakiwa wamekaa 
Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bw. Mhela Victor Mohamed akigawa cheti kwa mtihimu kwenye Mahafali ya 39 ya Chuo cha VETA Mkoa wa Shinyanga
Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bw. Mhela Victor Mohamed akiendelea kugawa vyeti kwa watihimu 

Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bw. Mhela Victor Mohamed akiendelea kugawa zawadi kwa watihimu 

Zoezi la kupeana zawadi likiendelea
Zoezi la kupeana zawadi likiendelea
Burudani ikiendelea
Picha ya pamoja Mgeni rasmi na Wahitimu wa mafunzo ya Hatua ya Pili (Level II) 

Picha ya pamoja Mgeni rasmi na Walimu wa chuo cha VETA

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

0/Post a Comment/Comments