Na Heri Shaaban (Ilala )
MBUNGE wa Jimbo la Ilala ,Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu amesema Mwaka 2025 katika Uchaguzi Mkuu Jimbo la Ilala wote wanamchagua Rais Samia Suluhu Hassan.
Mbunge Zungu alisema hayo Leo wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2020 /2022 Mgeni rasmi akiwa mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam Abbas Mtemvu .
"Wananchi wangu wa Jimbo la Ilala Naomba ushirikiano wenu tujenge misingi ya chama na kutekekeza Ilani na mgombea wetu wa Urais 2025 tiketi ya CCM Samia Suluhu Hassan"alisema Zungu
Mbunge Zungu amewaomba Ilala waweke ukurasa Mpya Udiwani na Ubunge watapata mda ukifika wasipite pite kufanya kampeni kwa sasa muda bado .
Akizungumzia Utekelezaji wa Ilani ya ccm aliyowasilisha alisema kila kata watapata Barabara za lami kwa asilimia 98 ,Hospitali ya kisasa ya mama na mtoto inajengwa Kata ya Mchikichini ambayo itatumika Ilala nzima inajengwa kwa fedha za tozo .
Alisema Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani kila kiongozi wa Chama atapata Taarifa ya Ilani kuangalia Utekelezaji wa ILANI taarifa ambayo Mbunge Zungu amewasilisha kwa njia ya mtandao
Akizungumzia changamoto ya Umeme kwa Sasa alisema MH,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan analifanyia kazi changamoto hiyo itakwisha hivi karibuni umeme utapatikana maeneo yote.
Post a Comment