MNAJIMU na Mkufunzi wa elimu ya dini ya Kiislam nchini Sheikh Sharif Ahmad Bawazir, ameitabiria Tanzania kupata mvua kubwa na zenye neema katika mwaka unaoanza kesho ambayo pamoja na kuleta faida kwa wakulima pia itasaidia kuongeza kina cha maji katika Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Bawazir anayefanya shughuli za kutoa mawaidha ya elimu ya dini ndani na nje ya Tanzania, pia amesema chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania itazidi kusonga mbele kimaendeleo kutokana na nyota nzuri aliyonayo huku akitolea mfano wa mambo mbalimbali aliyoyafanya tangu alipoapishwa kuwa Rais.
Amesema kutokana na namba ya mwaka ujao katika hesabu za kitabiri, inaonesha uwepo wa mvua za kutosha katika maeneo mbalimbali ya nchi ambazo kama zitatumiwa vizuri kwa kilimo zinaweza kuiletea Tanzania faida ya kuwa na chakula cha kutosha na hata kwa ajili ya biashara.
Kuhusu maendeleo , Sheikh Bawazir amesema kama ilivyojitokeza tangu Rais Dkt. Samia aingie madarakani, maendeleo ya Tanzania itazidi kupiga hatua kubwa katika mwaka unaokuja kutokana na maono aliyonayo kiongozi huyo huku akiwataka wasaidizi wote walio chini yake kutomuangusha
"Tangu ameapishwa kushika hatamu, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi ikiwemo kuitangaza kiutalii nchi ambapo kwa sasa tunshuhudia idadi kubwa ya watalii wakiingia nchini, amewezesha ujenzi wa vyumba vingi vya madarasa, zahanati,hospitali sambamba na miundombinu mbalimbali zikiwemo barabara" amesema Bawazir
Amesema mbali na hayo pia Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya uongozi wake ameweza kuifungua nchi kiuchumi na kuwezesha uwepo wa fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo kimsingi zimesaidia kuongezeka kwa fursa za ajira kwa watanzania wa kada mbalimbali.
Aidha amewataka watanzania kuongeza juhudi katika kufanya kazi ili kuchagiza maendeleo yao na nchi kwa ujumla na kutumia fursa mbalimbali zilizopo ili kujiletea maendeleo hayo huku akisistiza kuwa kinyume na hapo ni kujitia umasikini.
Sheikh Bawazir aliyerejea nchini hivi karibuni aliwahi kutoa utabiri wa mambo mengi katika uongozi wa Hayati Rais Dkt John Magufuli na utabiri huo kutimia kwa asimilia kubwa jambo lililomfanya kupata umaharufu wakati huo kabla ya kuondoka nchini kwa shughuli zake za kikaz
Post a Comment