MWONGOZO KUKABILIANA NA UKATILI MAENEO YA MIKUSANYIKO MBIONI KUKAMILIKA.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Bw. Juma Samwel, akifungua Kikao cha Wadau kutoka Wizara za Kisekta wanaopitia na kuboresha Mwongozo wa Utakatumika kukabiliana na Ukatili unaofanyika kwenye Maeneo ya Umma.
Kaimu Mkurugenzi wa Jinsia Badru Abdunuru akitoa Salaama za Utangulizi kabla yakumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua Kikao kazi hicho chakupitia Mwongozo wakukabiliana na Ukatili kwenye maeneo ya Mikusanyiko ya Umma ikiwepo kwenye Masoko.


Baadhi ya Wajumbe wanaopitia Mwongozo wa kukabiliana na Vitendo vya Ukatili kwenye Maeneo ya Umma.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na MJJWM, Dodoma

SERIKALI ipo mbioni kukamilisha Mwongozo wa uanzishwaji wa Madawati ya Kijinsia katika maeneo ya mikusanyiko ya watu, ambapo kukamilika kwake kutasadia kutokomeza Vitendo vya Ukatili kwenye maeneo hayo ikiwepo masokoni.

Mwongozo huo ambao utahusisha maeneo ya Masoko, Vituo vya Usafirishaji abiria, Mialo ya Samaki na Maeneo ya Bandari upo mbioni kukamilika mara baada ya wadau chini ya Uratibu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, wanawake na Makundi Maalum kukutana jijini Dodoma kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi huo Leo Desemba, 21, 2022,  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Juma Samweli amesema, kukamilika kwa Mwongozo husika itakuwa ni muarobaini wa kushughulikia masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Uwezeshaji wa wanawake kwenye maeneo yaliyolengwa. 

Juma ameongeza kuwa, ili kazi hiyo iwe na umiliki wa Sekta zote amewaagiza Wajumbe hao kutumia muda huo wa Siku tatu kikamilifu kutafakari kwa kina na kutoka na Mwongozo uliokamilika ifikapo Desemba 27, 2022.

"Kwa kuwa Serikali inafanya kazi zake kwa kushirikiana na Wadau, kupitia Taasisi ya Equality for Growth (EFG) 2019 kupitia mradi uliojulikana kwa Jina la ‘‘Mpe riziki sio Matusi’’ kuanzisha Mwongozo wa Kupinga Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia Masokoni, ambapo walifanikiwa kuyafikia masoko yapatayo 15 kwa Mkoa wa Dar es Salaam na masoko 6 kwa Mkoa wa Shinyanga" amesema Juma. 

Juma ameongeza kuwa, Maeneo hayo yamekuwa na malalamiko mengi ya vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni pamoja na lugha chafu za udhalilishaji, miundombinu mibovu ya utendaji kazi, kukosekana kwa Usawa wa ushiriki wa Wanawake kwenye nafasi za Uongozi na maamuzi,kutokuwa na mazingira salama ya watoto wanaofika kwenye maeneo hayo pamoja na kukosekana kwa madawati ya Kijinsia yanayoweza kusaidia wahangwa wanaofanyiwa Ukatili. 

Akimkaribisha Mgeni  Rasmi, kufungua Kikao hicho, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Badru Abdunuru alisema, kufikiwa kwa hatua ya Mapitio ya Mwongozo huo, ni hatua ya kujipongeza kwa kuwa kiu na hamu ya Serikali ilikuwa nikuona kuna kuwa na Mwongozo Mahtusi utakaoweza kusimamia suala la Ukatili kwenye maeneo ya Mikuaanyiko ya watu.

Awali akitoa Salaam za Utangulizi, Mratibu wa Mradi wa Mradi wa UNFPA, Yohana Sekimweri alisema, kama Wizara waliona ni Busara kuwaita Wadau kutoka Sekta mbali mbali ili kupokea Mchango wa Mawazo ambayo yatasadia kuuboresha Mwongozo uwe na Sura ya Kitaifa. 

Matokeo ya mwongozo huo ni tafiti ya Afya ya Mtoto na Viashiria vya Malaria (TDHS–2015/16) vilionesha kuwa 40% ya wanawake wenye umri wa miaka 15 - 49 wameshawahi kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kimwili na 17% wameshawahi kufanyiwa ukatili wa kingono. 

Vilevile, taarifa ya utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia, 2017 kuhusu ukatili uliopo maeneo ya vituo vya usafiri ulionyesha 77% ya wanawake wenye umri wa miaka 18-25 wamefanyiwa vitendo vya ukatili katika vituo vya usafiri.  Mwanamke mmoja kati ya wanawake watano wenye umri kuanzia miaka 15-49 katika Mkoa wa Dar Es Salam wamepitia ukatili wa kimwili, matumizi ya lugha zisizo sahii na kejeli.


MWISHO

0/Post a Comment/Comments