Pastor Ishiva J. Mgimba wa Kanisa la City Center International Church of Tanzania alipozungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es salaam
..............................
NA MUSSA KHALID
Kanisa la City Center International Church of Tanzania limewataka watanzania kuongeza jitihada za kuliombea Taifa ili liweze kuepukana na changamoto mbalimbali ikiwemo Masuala ya ukatili ambayo yamejitokeza katika Mwaka 2022.
Kauli hiyo imetolewa Leo jijini Dar es salaam na Pastor Ishiva J. Mgimba wa Kanisa la City Center International Church of Tanzania wakati akizungumza na kituo hiki akitambulisha Maombi Maalum ya shukrani ya siku tatu ya kuliombea Taifa kuanzia Leo mpaka Jumapili yanayofanyika kwenye Kanisa hilo lililopo Ukumbi wa zanzibar ndani ya maonyesho ya Sabasaba Dar es salaam.
Pastor Mgimba amesema kuwa malengo ya Maombi hayo ni kunyenyekea kwa bwana Ili kuliombea Taifa na kulivusha kuelekea Mwaka 2023.
"Nchi yetu kwa sasa inapita katika kipindi kigumu maisha ya kijamii Kwa ujumla hasa Kwenye Masuala ya ustawi wa kiafya hasa kwenye kipengele cha ukatili wa kijinsia kumekuwa na kilio kikubwa kwenye jamii kutokana na Matukio ya ukatili wa kijinsia watu wakidiriki hata kuwakatili watoto jambo ambalo limesababisha huzuni katika baadhi ya familia"amesema Pastor Mgimba
Aidha Pastor Mgimba amesema wameandaa maombi hayo ili kuangalia kwa nini matukio ya kikatili yanatokea kwenye nchi ambapo watalikabidhi kwa Mungu ili kuweza kuyaombea yasijitokeze kwa mwaka 2023.
Amesema kuwa wanakwenda katika maombi hayo kulikomboa na taifa na watu kwani maandiko yanasema ‘waliponywa walikouwa na haja ya kuponywa hivyo amewataka wananchi kuitikia wito wa kushiriki katika maombi hayo kwani ndio wakati wa kurudi kwa Mungu.
‘Sasa hivi watu wengi wanaangaika kiuchumi sababu Shetani amekamata uchumi za watu sababu wanafanya kazi lakini mafanikio hawayaoni lakini ndani ya Yesu Kristo shetani hawezi kukamata uchumi kwa sababu unalindwa na bwana’amesema Pastor Mgimba
Pastor Mgimba ameendelea kusema kuwa changamoto zinazojitoka kwa sasa wanadamu hawana hofu ya Mungu tena bali wanashetani ameweka roho kwao na anawatumikisha hivyo amewaomba kurudi katika nyumba za ibada kwa ajili ya kukemea changamoto hizo ziweze kuwaondoka.
Kuhusu ushirikiano na serikali ameiasa na kuikumbusha kutambua kuwa viongozi wa dini wananafasi kubwa sana hivyo wanapaswa kuthamini mchango wao katika kuliombea taifa na viongozi wake.
Maombi hayo yanaanza leo Dec 30 na yatahitimishwa Jumapili Januari 1,2023 baada ya kufanya ibada na kusudio lao ni kuhakikisha Taifa linakombolewa na bwana liendelee kuwa na amani wakati wote.
Post a Comment