UMOJA wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Njombe umempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia malengo ya kuanzishwa kwa chama hicho ikiwemo utaratibu wa kuwapata viongozi mbalimbali wa kitaifa wa chama hicho sambamba na wajumbe wa Kamati Kuu.
Mbali na hatua hiyo pia UWT Mkoa wa Njombe umempongeza Dk Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahaman Kinana pamoja na Makamu mwenyekiti Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa kushika nafasi hizo.
Akizungumza muda mfupi baada ya kukamilika kwa Mkutano Mkuu wa CCM Mjini Dodoma, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe Scolastika Kevela amesema maono ya Dk Samia Suluhu Hassan yamekuwa yakitimia siku Hadi siku hatua inayoonyesha dira ya Taifa la Tanzania ulimwenguni.
"Tunamshukuru Mungu tumemaliza salama mkutano Mkuu wa Chama chetu lakini kikubwa ni kwa mafanikio ya Chama chetu yanayoendelea kupatikana kupitia uongozi wa Rais na Mwenyekiti wa Chama chetu Taifa Dk Samia Suluhu Hassan ambaye tangu aanze kukiongoza chama hiki ameweza kusimamia vizuri malengo ya dira ya chama chetu" amesema Scolastika.
Miongoni mwa mambo ambayo Mwenyekiti huyo wa UWT Mkoa wa Njombe ameyaanisha kuwa Dk Samia Suluhu Hassan Rais na Mwenykiti wa CCM Taifa ameweza kuyasimamia ni pamoja na kutekeleza kikamilifu ilani ya Chama Cha Mapinduzi ikiwemo ujenzi wa miundombinu mbalimbali na mengineyo pamoja na kufanikisha chaguzi zote za ndani za chama hicho.
Alisema chaguzi za Mwaka huu za Chama hicho zilitawaliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wanachama wake wote waliokuwa wameonesha nia ya kuutaka uongozi kama taratibu za chama hicho zinavyotaka ambapo baadhi yao walofanikiwa kupata nafasi.
"Kwanza tunawapongeza viongozi wote wa ngazi ya juu kwa kuaminiwa kwao na wajumbe kwa niaba ya wanachama, lakini pamoja nao viongozi wote wa ngazi za mashina hadi Mkoa, haha ndiyo mafanikio mafanikio zaidi ndani ya chama ambayo Rais wetu Dk Samia Suluhu Hassan anayasimamia" ameongeza Mwenyekiti huyo Mkoa wa Njombe.
Aidha amesema kupitia kwa viongozi wote wa chama hicho waliochaguliwa kukingoza chama hicho katika nafasi mbalimbali kwa kipindi cha miaka minne ijayo, Imani yake CCM itaendelea kubaki imara na kuwa mfano dhidi ya vyama vingine na ndani na nje ya Tanzania kitu ambacho kwa miaka mingi tangu imekuwa ikifanya.
"Niwaombe viongozi wote kuanzia ngazi ya Chama Taifa hadi mashina wakiwemo wajumbe waliochaguliwa katika kamati mbalimbali kuendelea kuwa na umoja na mshikamano wakati wote lakini zaidi kumpa ushirikiano wa kutosha Dk Samia Suluhu Hassan katika kuliongoza Taifa hili" amesisitiza Scolastika.
Pamona na hayo amesema UWT Njombe itaendelea kusimama na Serikali inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan wakati wote anapoteleza majuku yake ya Chama na ya Taifa hadi atakapomaliza miula yake yote uongozi kikatiba.
Post a Comment