WASANII WANAOHAMASISHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KUWAJIBISHWA

 



Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya amewaonya wasanii wa Tanzania wanaotunga nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi na kusema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wasanii hao.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Desemba 7, 2022 jijini Dar es salaam Kusaya ameeleza kuwa hatua zitachukuliwa kwa wasaniii ambao hawatumii kipaji chao kuwaelimisha watu badala yake wanatunga nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya.

Katika hatua nyingine Mamlaka hiyo  imefanikiwa kukamata jumla ya kilo 16.643 za dawa za kulevya zikijumuisha kilo 15.19 za heroin, gramu 655.73 za Cocaine na gramu 968.67 za Methamphetamine zilizowahusisha jumla ya watuhumiwa saba.

” Watuhumiwa hawa ni Washirika  wa Kambi Zuberi Seif na wenzake waliokamatwa wakiwa na kilo 34.89 za heroin katika operasheni ya mwanzoni  mwa mwezi Novemba 2022″.  Amesema Kamishna Jenerali Kusaya.

Aidha amesema watuhumiwa hao watatu  ni Suleiman Thabiti Ngulangwa (36), mfanyabiashara na mkazi  wa Salasala,  Sharifa Seleman Bakar(41),  Mkazi wa Maji matitu-Mbagala , wote ni wakazi wa Dar es Salaam.

Hata hivyo amesema watuhumiwa wengine wanne walikamatwa wakiwa na gramu 655.75 za cocaine na gramu 968.67 za Methamphetamine.

 

 




0/Post a Comment/Comments