Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kwa kushirikiana na timu maalum ya kuzuia na kupambana na makosa ya mtandao limewakamata watuhumiwa 11 wa makosa ya kimtandao.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro Jumenne Muliro, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kukamatwa kwa wahalifu hao ni kufuatia ufuatiliaji mkali unaoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi, na Timu hiyo Maalum.
Katika hatua hiyo Jeshi la Polisi na timu hiyo, limemkamata Alex Magoti (26) Mkazi wa Tabora Mjini na wenzake nane kwa tuhuma za kumiliki Runinga za mtandaoni, na akaunti za mitandao ya kijamii ambazo zimekuwa zikitumika kusambaza taarifa za uongo au uzushi kuhusu Rais Dkt. Samia na viongozi wengine wakuu wa Serikali.
Katika hatua nyingine Kamanda Muliro amesema, wanamshikilia Li Naiyong (48) raia wa China, ambaye anatuhumiwa kujihusisha na shughuli za kuingilia mfumo wa mawasiliano kinyume na taratibu za nchi, na kuisababishia Serikali hasara ya kiasi cha Shilingi Milioni Mia mbili ishirini na moja laki moja sitini na tatu na mia sita (Tshs 221,163,600).
Post a Comment