xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kwa kushirikana na ofisi ya taifa ya mashitaka limefanikiwa limefanikiwa kuwafikisha mahakamani jumla ya watuhumiwa 270 kwa makosa ya ubakaji nawatuhumiwa wawili kati yao wamefungwa kifungo cha Maisha jela na wengine miaka thelathini kila mmoja.
Akitoa taarifa hiyo hii leo December 14 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishina msadizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO amesema kati ya watuhumiwa 270 watuhumiwa 223 walipatikana na hatia kati yao wawili ambao ni ni PETER LEONARD (27) mkazi wa lashaine Monduli kwa kosa la kubaka mtoto mwenye umri (07) na PAUL HILONGA (60) mkazi wa Karatu wote waili wamefungwa kifungo cha Maisha jela kwa kosa la kubaka.
Kamanda Masejo amewaambia waandishi wahabari kuwa Jeshi hilo liliendesha operesheni maaalum ambapo watuhuiwa 127 na pikipiki 125 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo taa mbazo zimepgwa marufuku,wenye namba bandia,Pamoja na pikipiki ambazo zimefutwa namba.A
meongeza kuwa pikipiki hizo zimekuwa kero kwa wananchi husasani wenye magonjwa mbalimbali nakubainisha kuwa Jeshi hilo linaendelea na msako mkali wa vyombo hivyo ambapoa amesema wanafanya utaratibu wa kimahakama kutaifisha pikipiki hizo.
ACP Masejo ametoa rahi kwa wananchi wa mkoa huo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo ili kukomesha vitendo vya kihalifu Pia amebainisha kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wamejipanga vyema sikukuu za mwisho wa mwaka.
Kwa upande wake Juma buruani amesema wao kama viongozi wa waendesha pikipiki wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kutoa rahi kwa wenza kuachana na vitendo ambavyo vitawafanya kukamatwa na Jeshi hilo.
Mwenyekiti wa waendesha pikipiki kutoka kata ya Murieti amesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa madereva wenzao ili kuwa nauwelewa wa Pamoja.
Post a Comment