xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi) Ludovick Nduhiye amezindua Mafunzo kwa Watumishi 43 Wa Vivuko Vinavyosimamiwa na TEMESA Katika Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI).
Akizungumza leo Desemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam amesema kupitia mafunzo hayo matarajio ni kuona maboresho makubwa katika uendeshaji wa vivuko vyetu nchini hivyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa makini katika kupokea mafunzo watakayopata na kwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo na hivyo kuboresha huduma za vivuko nchini.
"Katika kushiriki Mafunzo haya kulingana na fani zenu mnapaswa kutambua kuwa mnalo jukumu la kujifunza kwa bidii ili kuongeza kiwango cha uelewa wenu na hivyo kuboresha utendaji kazi katika maeneo yenu". AmesemaMtendaji Mkuu wa TEMESA Bw. Lazaro Kilahala amesema TEMESA ina jumla ya vituo 22 vyene jumla ya vivuko 33 kote nchini. Kila kivuko kinapaswa kuwa na manahodha, mabaharia, wahandisi pamoja na mafundi wenye sifa zinazoendana na sheria zinazoongoza vyombo vya majini.
Amesema kuwa Wakala utaendelea kutoa mafunzo hayo muhimu kadri ya mahitaji ili kuhakikisha vivuko vyetu vinahudumiwa na watumishi wenye sifa stahiki ili kupunguza changamoto ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.
“Kwa kutambua jitihada kubwa zilizofanywa na serikali katika kuhakikisha kuwa fedha kwa ajili ya mafunzo haya zinapatikana tumeona ni muhimu leo tuungane na Serikali katika kuutambua mchango mkubwa katika kufanikisha mafunzo haya”. Amesema
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Bw. Lazaro Kilahala amesema TEMESA ina jumla ya vituo 22 vyene jumla ya vivuko 33 kote nchini. Kila kivuko kinapaswa kuwa na manahodha, mabaharia, wahandisi pamoja na mafundi wenye sifa zinazoendana na sheria zinazoongoza vyombo vya majini.

Post a Comment