ZAIDI YA WATANZANIA 5000 WANAUGUA HIMOFILIA BILA KUJUA


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,Prof.Mohamed Janab akizungumza na waandishi wa habari jana Desemba 13,2022 Jijini Dar es Salaam. 
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu na Mkuu wa Kitengo cha Wagonjwa wa Damu Muhimbili Dkt.Stella Rwezaula akizungumza na waandishi wa habari jana Desemba 13,2022 Jijini Dar es Salaam.Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Dkt.Victor Mgotta akizungumza na waandishi wa habari jana Desemba 13,2022 Jijini Dar es Salaam.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kushirikiana na wataalamu kutoka nchini Kenya kufanya tohara salama kwa wagonjwa 25 wenye  changamoto ya uvujaji wa damu (HIMOFILIA).

Hatua hiyo ni kwa mara ya kwanza kufanyika ambapo kambi hiyo imeanza rasmi tarehe  12 na itahitimishwa tarehe 16 Desemba 2022 huku ikienda sambamba na utoaji wa mafunzo kwa wataalamu 8 kutoka hospitali mbalimbali za Tanzania zenye kliniki ya ugonjwa wa Himofilia.

Akizungumza mapema jana jijini Dar es  salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,Prof.Mohamed Janabi, amesema kuwa aina  hiyo ya upasuaji utafanyika kwa njia tofauti na ilivyozoeleka kwani wagonjwa hao wanahitaji uangalizi wa karibu ili kuepuka athari ya kupoteza damu,pia mgonjwa atahitajika kulazwa kw amuda wa siku tano hadi saba.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu na Mkuu wa Kitengo cha Wagonjwa wa Damu Muhimbili Dkt.Stella Rwezaula amesema kuwa kuwa zaidi ya watanzania 5800 wana tatizo la haemophinia bila kujua kuwa wanatatizo hilo.

Aidha Dkt.Stella amewashauri watu kuacha imani za kishirikina, wasiende kwa waganga wa kienyeji pale wanapomuona mgonjwa anayetokwa damu puani, au anayetokwa na damu isivyokawaida aking’olewa jino au baada ya kufanyiwa tohara n.k, bali waende kwa wataalamu wa afya ili wapewe matibabu sahihi.

Naye Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto Dkt.Victor Mgotta ametoa wito kwa wanaotokwa na damu bila udhibiti wajitokeze kwenye vituo vya afya vya kanda ili waweze kupatiwa matibabu.

Hoemophibia ni ugonjwa wa kutokwa damu bila ukomo, ambapo imeelezwa kuwa asilimia 70 ya wagonjwa hurithi kutoka kizazi hadi kizazi, na asilimia 30 hupata kutokana na mabadiliko ya vinasaba.







0/Post a Comment/Comments