Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi
Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha watakiwa kutojihusisha na ushabiki wa vyama vya siasa
Hayo yamesemwa leo Januria 09 2023 na kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Nchini kamishina Msaidiz wa Polisi ACP SIMON PASUA wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza askari walio fanya vizur zaidi mwaka jana 2022 Mkoani Arusha.
Kamanda Pasua amesema kuwa askari wanapaswa kushanikia maswala mengine ya kijamiii kama vile michezo amewataka askari hao kujikita zaidi katika ulinzi wa raia na mali zao ili kuleta ufanisi na kupunguza manunguniko ya wananchi.
Ameongeza kuwa waliopata zawadi wanaomuda wakuongeza juhudi ili mwaka mwingine waendele kupata zawadi hizo ikiwa ni pamoja na kupanda vyeo ambapo amewataka kufanya kazi kwa umoja ili kuleta ufanisi wa kazi za Polisi .
Kwa Upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishina msaidizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO amempongeza Kamanda wa kikosi hicho kwa kutambua mchango wa askari wanaofanya kazi vizuri zaidi kazini.
Kamanda Masejo amebainisha kuwa watanzania wanalitegemea sana Jeshi hilo ambapo amebainisha kuwa askari waliofanya vizuri wataliwakilisha vyema Jeshi ikiwa ni pamoja na wengine ambao wajapata zawadi hizo
Nae askari wa kikosi hicho kutoka Makao Makuu ya kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo Copolo wa Polisi CPL SILVESTER MANG’AHA aliye pata zawadi kwa kufanya kazi vizuri mwaka 2022 amewashukuru askari wenzake ambapo amebainisha kuwa kitendo cha kupata zawadi hiyo ni mchango na ushirikiano kutoka kwa askari wenzake.
Post a Comment