Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Ardhi na Nyumba la Wialaya ya Kinondoni limetoa amri ya zuio ya ujenzi wa Kituo cha Afya eneo la Tegeta 'A' Goba jijini Dar es Salaam.
Amri hiyo imetolewa tarehe 20 Disemba 2022 na Mwenyekiti wa Baraza hilo Longinus Rugarabamu baada ya waombaji kuwasilisha zuio hilo kupitia wakili wao Dickson Matata.
Maombi ya msingi kwenye shauri hilo ni kulitaka baraza litamke mmiliki halali wa eneo hilo na limkabidhi haki ya kisheria ya umiliki pamoja na kinga ya Mahakama sambamba na maombi madogo ya kuzuia ujenzi unaoendelea wa kituo cha afya unaondelea kwenye kituo hicho.
Waombaji wanadai kuwa uongozi wa Kata pamoja na Manspaa ya Kinondoni umechukua eneo hilo kimabavu bila kufuata sheria na kutoa haki kwa wamiliki .
Waombaji kwenye shauri hilo ni pamoja na Romanie Mosha Godfrey Roman, Rumishael Roman na George Mazewa na wadaiwa wakini ni Mtendaji wa Kata ya Goba, Manspaa ya Wilaya ya Kinondoni, Tabia Mziwanda na Mrisho Ramadhani.
Akitoa amri hiyo Mwenyekiti Rugarabamu alisema "Ombi la zuio hilo limekubaliwa wajibu maombi, watumishi au mawakala wao hawaturuhusiwa kufanya shughuli ya uendelazaji eneo hilo mpaka shauri la msingi litakapo sililizwa.
Awali mgogoro huo uliwahusu Familia ya Saidi Mziwanda na Romani Mosha ambao walikuwa wakivutana kuhusu mipaka ya shamba hilo, lakini katika Manispaa ya Ubungo ambao awali waliomba mahakama kujiondoa katika Mgogoro na kuanza kujenga kituo hicho cha Afya Goba bila kufuata taratibu za milki na kusababisha mvutano mkubwa kabla ya zuio lililopo hivi sasa
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Dokta Peter Nsanya amesema hana taarifa ya zuio hilo lakini kazi ya ujenzi itaendelea mpaka itakapopatikana taarifa rasmi katika ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa " Mimi sina taarifa ndugu mwandishi, lakini kazi itaendelea mpaka hapo nitakapopata taarifa rasmi ya zuio hilo" alimaliza
Post a Comment