BENKI YA ACCESS MICROFINANCE YAANZA MWAKA 2023 NA AKINA MAMA WANAOJIFUNGUA HOSPITALI YA KAHAMA

Afisa Mkuu wa Biashara wa Access Microfinance Bank, Bw. Isaya Mwenisongole (kushoto) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama Dkt. Deo Nyaga vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit) kwa ajili ya akina mama wanaojifungua katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.

Wafanyakazi wa Access Microfinance Bank na wafanyakazi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama wakiwa wameshikilia vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit) vilivyotolewa na Access Microfinance Bank kwa ajili ya akina mama wanaojifungua katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Benki ya Access Microfinance Tanzania imetoa msaada wa vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit) na sabuni kwa akina mama katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto.

Vifaa hivyo vya kujifungulia pamoja na sabuni za unga za kufulia zimekabidhiwa leo Jumamosi Januari 14,2023 na Afisa Mkuu wa Biashara wa benki ya Access  Microfinance , Bw. Isaya Mwenisongole kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama Dkt. Deo Nyaga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mwenisongole amesema benki ya Access Microfinance  imekuwa na utamaduni wa kusaidia jamii na kwamba mwaka huu mpya 2023 wameona ni vyema kuanza na akina mama wanaojifungua katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.

“Sisi Access Microfinance Bank utamaduni wetu ni kusaidia jamii ndiyo maana tumeamua kufungua mwaka mpya 2023 kwa kutoa hiki kidogo  kwa ajili ya akina mama wanaokuja kujifungua kwenye hospitali hii ya Kahama ikiwa ni sehemu pia ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya afya nchini”,amesema Mwenisongole.

“Tumekabidhi uongozi wa hospitali ya Manispaa ya Kahama vifaa vya kujifungulia (Delivery kit) maboksi matano yenye vipande (piece) 18 kila moja na sabuni za unga za kufulia maboksi manne vyote vikiwa na thamani ya shilingi 1,400,000/= ambapo akina mama wanaofika kujifungua watakuwa wanapatiwa. Lakini pia tumegawa sabuni kwa akina mama waliolazwa hospitali”,ameeleza Mwenisongole.

Akipokea vifaa hivyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama Dkt. Deo Nyaga ameishukuru Access Microfinance Bank Tanzania kwa kuwajali akina mama huku akiwaomba wadau wengine kuiga mfano wa benki hiyo.

“Tunawashukuru Access Microfinance Bank kwa jambo hili la utu, mmefanya tendo la huruma vifaa hivi vya kujifungulia vitawasaidia akina mama ambao wanafika hapa bila ndugu. Vifaa hivi tutawapatia bure akina mama wenye uhitaji wanaokuja kujifungua”,amesema Dkt. Nyaga.

“Vifaa hivi ni muhimu  naomba wadau wengine waje kusaidia kwani mahitaji ni makubwa ikilinganishwa kuwa kwa mwezi akina mama wanaojifungua kwenye hospitali hii ni wengi. Kwa mwezi tunazalisha kwa njia ya kawaida akina mama zaidi ya 200 na kwa njia ya upasuaji ni kati ya 40 hadi 60”,ameongeza Dkt. Nyaga.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Muonekano wa sehemu ya vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit) na sabuni vilivyotolewa na Access Microfinance Bank katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga leo Jumamosi Januari 14,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Afisa Mkuu wa Biashara wa Access Microfinance Bank, Bw. Isaya Mwenisongole akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit) na sabuni vilivyotolewa na Access Microfinance Bank kwa ajili ya akina mama wanaojifungua katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga
Afisa Mkuu wa Biashara wa Access Microfinance Bank, Bw. Isaya Mwenisongole akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit) na sabuni vilivyotolewa na Access Microfinance Bank kwa ajili ya akina mama wanaojifungua katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama
Afisa Mkuu wa Biashara wa Access Microfinance Bank, Bw. Isaya Mwenisongole (kushoto) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama Dkt. Deo Nyaga vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit) vilivyotolewa na Access Microfinance Bank kwa ajili ya akina mama wanaojifungua katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.

 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama Dkt. Deo Nyaga  akizungumza wakati akipokea vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit) vilivyotolewa na Access Microfinance Bank kwa ajili ya akina mama wanaojifungua katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama Dkt. Deo Nyaga (wa nne kulia) akiangalia vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit) vilivyotolewa na Access Microfinance Bank kwa ajili ya akina mama wanaojifungua katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.
Wafanyakazi wa Access Microfinance Bank na wafanyakazi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama wakiwa wameshikilia vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit) vilivyotolewa na Access Microfinance Bank kwa ajili ya akina mama wanaojifungua katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.
Wafanyakazi wa Access Microfinance Bank wakiwa wamebeba mifuko ya sabuni za kufulia wakielekea kwenye wodi ya akina mama waliolazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama kwa ajili ya kuwagawia.

Mfanyakazi wa Access Microfinance Bank akimpa sabuni mama aliyelazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama
Afisa Mkuu wa Biashara wa Access Bank Microfinance, Bw. Isaya Mwenisongole akimpa sabuni mama aliyelazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama
Mfanyakazi wa Access Microfinance Bank akimpa sabuni mama aliyelazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama
Wafanyakazi wa Access Microfinance Bank wakiendelea kugawa sabuni kwa akina mama waliolazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama
Meneja wa Access Microfinance Bank Tawi la Kahama, Bw. Elikana Manyanza akiangalia vifaa vya kujifungulia
Wafanyakazi wa Access Microfinance Bank wakiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama
Wafanyakazi wa Access Microfinance Bank wakiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama
Wafanyakazi wa Access Microfinance Bank wakiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

0/Post a Comment/Comments