Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Kashindye Mlolwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Januari 7,2023 katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Kashindye Mlolwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Januari 7,2023 katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Kashindye Mlolwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Januari 7,2023 katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Kashindye Mlolwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Januari 7,2023 katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga kimempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazozifanya kwa Watanzania ikiwemo kupanua wigo wa Demokrasia Diplomasia huku kiviomba vyama vya Upinzani nchini kusema ukweli kuhusu maendeleo yaliyofanywa na serikali.
Pongezi hizo z imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Kashindye Mlolwa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Januari 7,2023 katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga.
“Tunampongeza sana Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazozifanya kwa Watanzania hasa kwenye suala la Demokrasia na Diplomasia kwa ujumla, hivi karibuni ametoa tamko la kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vyote vya siasa ikiwa ni moja ya tunda la maridhiano, jambo ambalo litaleta chachu ya Demokrasia na Ushindani wa kisiasa kwa hoja katika nchi yetu”.
"CCM Mkoa wa Shinyanga tunampongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupanua wigo wa Demokrasia Tanzania, ameruhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya upinzani (Vyama Rafiki). Mikutano hii ya hadhara italeta chachu, twendeni tukashindane kwa hoja, sisi tumejipanga kwa mikutano, Moto umeshawashwa tutawapa ratiba ya mikutano, sisi tumejipambanua kwa Ilani yetu, hatuna Presha".
"Siasa siyo uadui, siasa ni kujenga amani ya nchi. Vyama vya siasa vikifika kwenye maeneo waseme tu ukweli wa mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali. Vyama Rafiki wakiri ukweli wa mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali visifunike miwani ya mbao kwenye ukweli, waseme tu ukweli mambo makubwa yamefanyika", amesema Mlolwa.
"Hili la vyama vya siasa visifanye mikutano kwamba tulikuwa na hofu gani, hata sisi CCM lilituathiri na CCM. Hii Pin ya kutofanya mikutano ilituhusu pia, sasa tupo tayari kwenda kufanya mikutano ya hadhara na hili ni agizo la Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kilichobaki sasa ni utekelezaji tu Sisi tuna Ilani ya Uchaguzi ya CCM tunayoisimamia kazi yetu ni kutekeleza tu", ameongeza Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga.
Ameeleza kuwa, mbali na kupanua wigo wa Demokrasia, Pia Rais Samia amefanya mambo makubwa kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisas itakayonufaisha pia wakazi wa Shinyanga na mambo kadha wa kadha.
“Tunampongeza Mhe. Rais Samia kwa mvua ya maendeleo mkoa wa Shinyanga. Mama Samia ni kiongozi na Rais wa mfano, ni mama mwenye huruma mwenye upendo mkubwa kwa Watanzania, amejenga shule za watoto wa kike waweze kusoma hata waliopewa ujauzito na kujifungua, ameleta tumaini kwa watoto wa kike Tanzania”,amesema.
“Miradi yote ya kimkakati inaendelea kwa kiwango cha hali ya juu. Pia tunampongeza Mhe. Rais Samia kwa miradi inayoendelea kujengwa nchi nzima. Hivi karibuni tumeona ujazaji wa maji katika bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere huko Rufiji. Pia tumeshuhudia ujenzi wa madarasa mbalimbali kwenye maeneo yenye uhitaji nchi nzima, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya,ujenzi wa barabara za rami,kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita, kujali maslahi ya watumishi wa umma na mengine mengi”,ameongeza Mabala.
Post a Comment