DKT MPAMGO KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA SGR TABORA ISAKA

 



Na Richard Mrusha 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango anatarajia kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR Tabora _Isaka ambapo mradi huo utakuwa ni kuhitimisha awamu ya kwanza ya mradi kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza .

Mradi huo wa SGR Tabora _Isaka utahusisha ujenzi wa reli yenye kiwango cha kimataifa SGR Kwa urefu wa kilomita 165 ikijumuisha kilomita 130 njia kuu na kilomita 35 za njia za kupishana  .

Akizungumza mbele ya waandishi wa  Habari Mkurugenzi mkuu wa shirika la TRC Masanja kadogosa Januari 16 mwaka 2023 Mkoani Shinyanga Wilaya ya kahama ndani ya halmashauri ya Msalala  amesema mradi  wa SGR kipande cha Tabora _Isaka ni utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa SGR Dar es Salaam _Mwanza ( km 1,219) yenye vipande vitano Dar es Salaam _Morogoro ,Morogoro _Makotopora .

Masanja ameongeza kuwa kipande kingine ni Makotopora _Tabora ,Tabora _Isaka na Isaka_hadi kufika Mwanza  na ujenzi wa reli hiyo ya kisasa utaendelea kuleta faida Kwa wananchi na taifa Kwa ujumla ikiwemo upatikanaji wa fursa za Moja Kwa Moja kupitia Kampuni ,wajasiriamali  wadogo na wafanyabiashara .

Shirika la reli Tanzania limeandaa  treni mbili maalumu siku ya Januari 18 2023 itakayobeba wananchi kutoka stesheni ya Tabora saa 11:00 asubuhi  na kutoka Shinyanga saa 12 : 00 asubuhi kuelekea Isaka na baadae kurudi Tabora na Shinyanga baada hafla kuisha .

Shirika hilo linawakaribisha wananchi wote hususani Kanda ya ziwa  kuhudhuria tukio hilo la kihistoria la uwekaji  wa jiwe la msingi .

Mwisho.

0/Post a Comment/Comments