FORUM CC - SEKTA YA KILIMO NA UFUGAJI NDIZO ZINAZOATHIWA ZAIDI NA ATHARI ZA MABADILIKO TABIA NCHI.


 .........................

TAARIFA NA SALIM BITCHUKA

Imeelezwa kuwa bado Changamoto za mabadiliko ya tabia nchi zinawaathiri wakulima hususan vifaa ambavyo vingetumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Afisa miradi kutoka jukwaa la mabadiliko ya tabia nchi (Forum CC) Msololo Onditi wakati wa mkutano uliohusisha utazamaji makala iliyoonyesha umuhimu wa shuguli endelevu katika ufufugaji nyuki, ufugaji samaki,kilimo na kilimo cha mbogamboga.

Msololo Onditi amesema vifaa vinavyotumika katika kilimo cha umwagiliaji ni gharama huku kukiwa na kilio cha elimu ya watu kutoweza kutumia vifaa hivyo na uaminifu wa teknolojia hiyo kuwa ni mdogo .

Kwa upande wao baadhi ya washiriki Dkt. Prosper Masawe kutoka tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Bettie Luwugu kutoka shirika la kuhifadhi misitu ya Asili Tanzania kwa pamoja wamesema kama nguvu itaongezwa zaidi katika kuielimisha jamii kutasaidia kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuongeza ujumuishi wa vijana na akina mama kwenye harakati za kukabiliana na hali hiyo.

Mkutano huo wa siku moja umehusisha Asasi zisizo za Kiserikali,taasisi za elimu ya juu,watafiti na wanahabari ukiwa na lengo la kuangalia shughuli endelevu katika sekta za kilimo na ufaugaji ikiwa ni sekta ambayo inaathiriwa zaidi na athati za mabadiliko ya tabia nchi.

0/Post a Comment/Comments