HALMASHAURI ZAHIMIZWA KUNUNUA DAWA ZA KUUA VIWADUDU,NDC WANATOA NENO.

 



Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

HALMASHAURI nchini zimetakiwa kuongeza kasi ya kununa Dawa za kuua viwadudu kwa ajili ya kumaliza mazalia ya Mbu na kuweza kutokomeza ugonjwa wa Maralia.

Rai hyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Rasilimari watu wa Shirika la maendeleo la Taifa(NDC),Harson Jacksoni,wakati zoezi la umwagiliaji dawa za viwadudu katika mitaa na madimbwi ndani yaKata ya Mabibo mtaa wa Relini Jijini Dar es Saalam ikiwa ni sehemu ya shirika ilo kurudisha kwa jamii.

Aidha,Jacksoni amesema licha halmashauri kuhimizwa na viongozi wa serikali kununua dawa kuuwa viwadudu lakini bado kasi hailizishi katika kununua dawa hizo na kuzitaka halmashauri kuongeza kasi katika manunuzi ya dawa hizo ili kuweza kuushinda ugonjwa wa Maralia.

Kwa Upande wake Mtaalamu wa Viwadudu kutoka Kiwanda cha viwadudu mkoani Pwani Baotic Product,John Tusiwe,amesema kiwanda hicho kizalisha dawa za kisasa na bora kwa ajili kuuwa mazalia ya mbu  ambazo zitasaidia  kuondokana na ugonjwa wa maralia.

Naye Afisa Uhusiano wa shirika la maendeleo Taifa (NDC),Amina Sanga,amezitaka Taasisi,watu binafsi kujitokeza katika kununua Dawa za kuua mazalia ya Mbu na akisema shirika ilo limejipanga kutoa elimu sehemu mbalimbali nchini juu ya umuhimu wa dawa hizo huku Wananchi wa kata ya mabibo wakiipongeza hatua ya NDC kumwaga dawa na kutaka zoezi hilo liwe endelevu

0/Post a Comment/Comments