KAMPUNI YA PARIMATCH YAMKABIDHI GARI MSHINDI WA CHOMOKA NA NDINGA


Mkurugenzi wa Kampuni ya Parimatch Tanzania Erick Gerald wakati akieleza mafanikio waliyoyapata katika Promosheni ya Chomoka na Ndinga kutoka Parimatch.

Afisa wa Mauzo kutoka Kampuni ya Toyota Tanzania Shamim Omary akilizungumzia gari ya aina ya Toyota Urban Cruiser ambalo kwa kushirikiana na Kampuni ya Parimatch Tanzania wamempatia mshindi Hamidu Abdallah.

Afisa Masoko wa wauzaji na wasambazaji wa Pikipiki za HIRO Hanter Norah Mapunda akielezea kuhusu washindi wa pikipiki walivyopatikana.

Mshindi wa gari ya aina ya Toyota Urban Cruiser Hamidu Abdallah akisema zawadi aliyoipata imetokana na juhudi katika ushiriki wa kampeni hiyo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Parimatch Tanzania Erick Gerald (kushoto) akimkabizi mshindi wa gari ya aina ya Toyota Urban Cruiser gari ambalo amelishinda

...........................

NA MUSSA KHALID

Kampuni ya Parimatch Tanzania imewashauri watanzania kuendelea kubashiri na parimatch ili waweze kunufaika na zawadi mbalimbali zitakazo wasaidia katika biashara au shughuli zao.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Erick Gerald wakati akieleza mafanikio waliyoyapata katika Promosheni ya Chomoka na Ndinga kutoka Parimatch ambayo imehitimishwa mwishoni mwa mwaka jana. 

Gerald amesema kuwa kupitia Promosheni hiyo imefanikiwa kumpata mshindi Hamidu Abdallah ambaye amekabidhiwa gari aina ya Toyota Urban Cruiser yenye thamani ya Sh Million 65.

‘Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki cha mwaka mpya kumkabishi mshindi wetu wa gari ya aina ya Toyota Urban Cruiser,gari hii ni jipya kabisa yaani zero kilomita hivyo tunawashukuru wateja wetu nchi nzima walioshiriki kwenye promosheni hii ya siku 35 ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi wa Disemba 2022’amesema Gerald 

Amesema kuwa Parimatch imekuwepo nchini tangu mwaka 2019 ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka,odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka,kasino na Michezo ya Virtual. 

Kwa upande wake Afisa wa Mauzo kutoka Kampuni ya Toyota Tanzania Shamim Omary amesema kuwa gari waliompatia mshindi huyo litakwenda kumsaidia katika matumizi yake ya kila siku kutokana na kuwa na gharama nafuu. 

Naye Afisa Masoko wa wauzaji na wasambazaji wa Pikipiki za HIRO Hanter Norah Mapunda amesema wataendelea kushirikiana na Parimatch kutoa zawadia Huku Mshindi wa Gari Hamidu Abdallah akisema zawadi aliyoipata imetokana na juhudi katika ushiriki wa kampeni hiyo.

Hamidu amesema kuwa wakati anapigiwa simu alikuwa nyumbani amelala kwani nyakati hizo kulikuwa na mvua hivyo hakuweza kuamini kwa haraka na alipopigiwa tena simu hakutegemea kama angeibuka mshindi.

Promosheni hiyo imedumu kwa siku 35 tangu Nov 22 hadi Disemba 26 mwaka jana ambapo imewapa nafasi wateja kujishindia zawadi mbalimbali.

0/Post a Comment/Comments