MGODI WA CANUCK WAIOMBA SERIKALI KUWAONDOA WACHIMBAJI WADOGO WALIOVAMIA KWENYE LESENI YAO.

 

Meneja rasilimali watu na utawala, David Deogratius akizungumza na waandishi wa habari


Xxxxxxxxxxxxxx

Na Richard Mrusha  Kahama 

 MENEJA  Rasirimali watu na utawala wa Kampuni ya Mgodi wa CANUCK uliopo Wilaya ya Msalala  kata ya Mwakanta kijiji cha Magung'humwa mkoani Shinyanga David  Deogratius amesema kuwa kampuni hiyo ilipata leseni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika kijiji hicho mwaka  2020  julai 30 na baada ya kupata leseni hiyo walianza shughuli za uchimbaji wa madini mara moja.

Amesema kuwa mwezi semptemba mwaka 2020 waliaza kuwasha mitambo kwa majaribio ya shughuli za uchakataji wa dhahabu na hadi sasa wanaendelea na shughuli hizo za uchimbaji wa madini ya dhahabu.

Deogratius ameyasema hayo mgodini hapo mwishoni mwa wiki wakati alipo tembelewa na  wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kwa lengo la kujifunza shughuli za uchimbaji wa madini ,ambapo amesema tangu wameaza shughuli za uchimbaji wa dhahabu katika eneo hilo la kijiji cha Magung'humwa kampuni hiyo imekuwa ikishiriki kwenye shughuli za mbalimbali kwenye jamiii inayowazunguka ikiwemo kushiriki moja kwa moja kwenye ujenzi wa shule ya msingi Magung'humwa.

Amesema kuwa wanafanya hivyo ikiwa ni sehemu juhudi zinazofanywa na jamii  katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ndani ya kijiji hicho ambayo wanayaazisha lakini pia licha ya kijiji hicho pia wamekuwa wakisaidia kwenye ujenzi wa maendeleo kwenye vijiji vingine ndani ya wilaya hiyo hata kabla ya kuingia kwenye mfuko wa maendeleo (CSR)  na wanafanya hivyo kadri wanavyopokea maombi kutoka kwenye maeneo hayo.

Meneja huyo akitolea mfano wa moja ya vijiji ambavyo  vimeendelea kunufaika uwepo wa mgodi huo ni pamoja na kijiji cha Numbi ,kagongwa na isaka kote huko walipokea maombi ya kusaidia shughuli za maendeleo ikiwamo ujenzi wa mashimo ya vyoo vya wanafunzi katika shule ya msingi Numbi ilipo katika kijiji cha Numbi na katika kata ya isaka kuna ujenzi wa kituo kipya cha polisi kampuni ya CANUCK baada ya kualikwa kama wadau wamaendeleo waliweza  kufika na kuchangia  nondo 70, lakini mbali na hapo kampuni hiyo wameweza kuweka miundombinu ya maji safi na salama eneo linalozunguka mgodi kwa ajili ya wananchi kuweza kupata huduma hiyo bure.

Ameongeza kuwa kwa mwaka 2021 /22 waliweza kukaa na serikali ya kijiji licha ya kwamba ndio wameaza kazi lakini walikubaliana kutenga kiasi cha fedha shilingi milioni 30 kwa lengo la kusaidia shughuli za maendeleo na miradi bunifu ambayo itaibuliwa na serikali ya kijiji na wamekuwa wakifanya hivyo mfano katika milioni 30 ya mwaka huo kampuni iliweza kulipa shilingi milioni tano katika ununuzi wa ardhi kwa ajili ya matumizi ya kujenga kituo cha afya cha kijiji cha Magung'humwa na hivi karibuni kampuni imeweza kulipa kiasi cha shilingi milioni 7.5 ili kusaidia ujenzi wa jengo la kituo cha afya.

Amefafanua kuwa katika eneo la ajira Kampuni hadi hivi sasa imeweza kutoa ajira ya kudumu kwa wafanyakazi 270 na licha wafanya kazi hao lakini wameendelea kutoa ajira hizo hususani katika eneo la uchimbaji  wameongeza waafanyakazi 51 ambao wanakwenda kuanza kazi katika idara ya (MINING) na idara ya uzalishaji na kwenyewe wanakwenda kuongeza wafanyakazi 35  na katika uchimbaji kuna njia zinaongezeka  za utafutaji dhahabu hivyo kunahitaji wafanyakazi.

Meneja huyo  ameongezeka kutokana na uzalishaji wameanzisha zamu tatu kwa wafanyakazi na wanahitaji wafanyakazi 70 hadi 100 hivyo kwa kiwango cha chini Kampuni inatarajia kuwa na wafanyakazi 350 mpaka 400 na hadi kufikia sasa inawafanyakazi 270.

wakati huohuo amesema kuwa kampuni yao ilipewa leseni ya uchimbaji lakini ndani ya leseni hiyohiyo kuna uvamizi wa wachimbaji wadogo ambao wanatambua kabisa kuwa Kampuni ya CANUCK ilishapewa leseni ya uchimbaji  lakini kwa kuzingatia mahusiano wanaomba mamlaka husika kuliangalia suala hilo na kuweza kupata ufumbuzi mapema kabla ya wale watu hawajafanya uwekezaji mkubwa ambao unaweza kuathiri uzalishaji wao.

Amesema kuondoka kwa watu hao kutawezesha kampuni  yao kuweza kuongeza uzalishaji kwa maana uwezo wa kampuni kuzalisha zaidi  kwani kushoto kwa mgodi wao kuna leseni ya watu wengine na kulia pia kuna leseni ya watu wengine na mbele yao kuna wachimbaji wadogo ambao wamevamia hivyo wanajikuta wako katikati na wanashindwa kujitanua ukizingatia leseni yao imefika hadi huko.

"Niombe pia kupaza sauti kwa serikali kupitia Wizara ya Madini ,keweza kusadia kulisukuma jambo hili japo kuwa tunapata ushirikiano mzuri kutoka kwa kamishna mkazi wa mkoa wa kimadini  Kahama na mkuu wa wilaya ya kahama Festo Kiswaga lakini tunaamini tutafanikisha kwa wakati hali ambayo itaongeza uzalishaji  na tukiweza kuzalisha zaidi tutaweza kurudisha kikubwa kwa jamii inayotuzunguka katika mfuko wa CSR ."amesema Deogratius

0/Post a Comment/Comments