Mizungu awataka vijana Ilala kusimama kidete katika miradi ya Chama




 ........................

Na Heri Shaaban (Ilala )

MWENYEKITI wa  Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Ilala Juma  Mizungu, amewataka vijana  kusimama kidete kumsaidia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,  kutekeleza  Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM  katika kusimamia miradi ya maendeleo .

Mwenyekiti Juma Mizungu aliyasema hayo Kata ya Kisutu Wilayani Ilala wakati wa matembezi ya hisani kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan .

"Nawahimiza vijana wangu kuanzia ngazi ya tawi,Kata na ngazi ya Umoja wa vijana wilaya  kutokusubiri vyama vya upinzani kukosoa  ndipo mjibu badala yake wayazungumzie  maendeleo yaliyopo  jamii ifahamu kwa kina miradi inayotekelezwa na Rais Samia  " alisema Mizungu 

Mizungu alisema Miradi ipo kuanzia ngazi ya mitaa yetu. Kiongozi wa UVCCM katika ngazi hiyo ni lazima uiseme  wananchi wa eneo lako wajue serikali inavyotekeleza kwani  umoja huo una  mchango mkubwa kuhakikisha  serikali inatekeleza Ilani ya CCM kwa asilimia  100.

“Katika Wilaya ya Ilala, serikali chini ya Rais Dk. Samia, imetekeleza miradi mingi. Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Kivule, vituo vya afya nane vinajengwa, ujenzi wa madarasa zaidi ya 300 , barabara na  huduma ya maji,”alieema  Mizungu.

Alipongeza UVCCM Kata ya Kisutu kwa kuandaa matembezi hayo maalumu kumpongeza Rais Dk. Samia  jambo alililosema litamtia moyo Rais kuendelea kufanya vizuri zaidi.

Katibu wa Mafunzo na Chipukizi wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Ummy, alisema vijana wawe mstari wa mbele kumuunga mkono Rais Dk. Samia kwani wao ndiyo wanufaika wakubwa wa miradi inayotekelezwa kuliko wazee.

“Mikutano ya vyama vya siasa imefunguliwa. hoja za wapinzani sasa zitakuwa ni kuikosoa serikali. UVCCM tusisubiri kujibu  hoja hizo bali  tuseme kabla hawajasema.

Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kisutu  Kumail Rizwani alisema  matembezi  hayo yalilenga kumpongeza Rais Dk. Samia, kutokana na kasi kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuboresha uhusiano wa kidipromasia na kupanua wigo wa demokrasia nchini.

0/Post a Comment/Comments