"MTUPE MUDA TUNAFUATILIA MAMBO YOTE NA TUTACHUKUA HATUA"-RAIS DKT.MWINYI

 




Xxxxxxxxxxxxx

Na. Andrew Chale,

Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba Wananchi wawe na subra kwani mambo yote  Serikali inafuatilia na inayafanyia kazi kwa mujibu wa kisheria za Nchi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari na Wahariri wa vyombo vya Habari, ikiwa ni muendelezo wake wa kuzungumza na Waandishi kila mwisho mwa mwezi, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 31-12-2022, akijibu maswali ya Waandishi ikiwemo suala la 'Video' inayotembea mitandaoni juu ya Mwananchi wa Zanzibar akieleza kuwa alifanyiwa vitendo vya utesaji kwa kile alichokitaja kuwa  alifanyiwa vitendo hivyo na Vikosi vya SMZ.

Akijibu swali hilo:

"Video Mimi nimeiona. Watu wanalalamika, nataka kusema kuwa vyombo vya Ulinzi vinaendelea kulinda raia na mali zao hivyo tupeni muda tutafanyia kazi uchunguzi na mtu akibainika wa Ulinzi na Usalama, atachukuliwa hatua" amebainisha Rais Dkt Mwinyi.

Aidha, amesema kuwa, Serikali pia inafuatilia suala la watu wanaojihusisha na vitendo vya kupiga na kupora watu 'Panya Road'  kwa Zanzibar,

Katika hatua nyingine, Rais Dkt Mwinyi amempongeza Mkuu wa Mafunzo kwa hatua aliyoichukua ya kuwasimamisha kazi watumishi kadhaa kufuatia kutoroka kwa Wafungwa na mahabusu.

Ambapo imeelezwa kuwa, kumekuwa na matukio ya kutoroka Wafungwa na Mahabusu hali ambayo inaleta wasiwasi kwa Jamii visiwani hapa baada ya hivi karibuni kutokea kwa matukio hayo.

Rais Dkt Mwinyi pia amesema kuwa, katika kupambana na suala la kuzuia vitendo vya unyanyasaji kwa watoto, ni kuhakikisha wanafunga mifumo thabiti ikiwemo kuwa na vifaa vya kisasa kama mashine ya DNA 

"Ushahidi mzuri ni WA DNA.

Hapa Zanzibar tunamashine tayari za DNA, hivyo ni kuwa na watu wenye ujuzi na weredi wa katika vyombo vyetu vitafanya kazi nzuri.

Mwisho.

0/Post a Comment/Comments