NDUGU wawili wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu wameiomba Serikali kuingilia kati dhuluma wanayofanyia katika nyumba ya familia ambayo ni urithi kutoka kwa Mama yao.
Wakizungumza kwa nyakati ndugu hao Jasmine Mtemvu na Ibrahim Mtemvu, wanasema wanashangazwa na kitendo cha mtu (Mhindi) anayedaiwa kuuuziwa nyumba hiyo ya ghorofa moja iliyopo Mtaa wa Haile Selasie Masaki na Kaka yao Abbas Mtemvu bila ridhaa ya wana familia wengine hali inayowafanya wabaki wakihangaika.
Walisema pamoja na kwenda mahakamani kupata haki yao, kesi iliyofunguliwa katika kituo Jumuishi cha Haki juu ya masuala ya familia kituo cha Temeke ambacho Novemba 28 Mwaka 2022 kutoa uamuzi wa kutofanyika kitu chochote katika nyumba hiyo na mtu huyo anayedaiwa kuuziwa, wadaiwa hao walikaidi agizo hilo na kuivunja nyumba hiyo.
"Tunaiomba Serikali iingilie kati dharma hii, nyumba ya familia inakuaje mtu mmoja anaiuza bila ridhaa ya wanafamilia wengine, mbaya zaidi mtu aliyeuziwa ambaye ni mhindi tunasikia naye ameenda kutufungulia kesi ya madai, haki ipo wapi wakati sisi ndiyo wenye mali" amesema Jasmine
Aidha amesema wao hawana tatizo na ndugu yao(Abbas) ila wanachoomba nyumba hiyo irudishwe katika umiliki wa familia kwa kuwa ni urithi wao kutoka kwa marehemu mama yao hivyo ni faida ya wote kama familia na siyo mtu mmoja.
"Tunachoshangaa na hatua ya mtu ambaye anatajwa kuwa mnunuzi mwenye asili ya Kihindi kwenda Mahakamani na kutufungulia kesi ambayo kwa mara ya kwanza tulikuwa mahakamani Januari 6 Mwaka huu, huu ni uonevu" alisema Jasmine.
Kwa upande wake Ibrahim Mtemvu amesema wakati wanasubiri hukumu ya kesi hiyo Machi 23 Mwaka huu, wanaiomba SeY,rikali kuhakikisha haki inatendeka kutokana na ukweli kuwa wanaona mwenendo wake tangu ilipoanza imetawaliwa na dalili za uwepo wa rushwa inayofanya haki yao kuchelewa.
Akisisitiza hilo amesema wapo tayari kutoa ushirikiano wa aina yeyote kwenye mamlaka zinazohusika ili waweze kuipata haki yao hiyo ambayo kwa sasa wanaona kabisa kuwa inapotea kutokana na mazingia yaliyopo.
Anasema kwa sasa wamelazimika kuishi kwa majirani baada ya kuondolewa kwa nguvu ndani ya nyumba hiyo ambayo imeshavunjwa na mhindi aliyeuziwa na ndugu yao.
Ends
Post a Comment