POLISI ASHIKILIWA KWA KOSA LA KUMSHAMBULIA MTOTO WAKE .


.............

Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linamshikilia askari wake Abati Benedicto Nkalango kwa kumshambulia mtoto wake wa miaka saba ,ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza kwa kumchapa kwa viboko na kumsababishia majeraha makubwa mwilini mwake. 

Kitendo Hicho Kimemsababishia Mtoto Huyo Kuvuja Damu Nyingi Mgongoni Na Masikioni Kufatia Majeraha Aliyoyapata Mtoto Huyo 

Kamanda Wa Polisi Mkoani  Simiyu Balasius Chatanda amesema tukio hilo limetokea januari 15 majira ya saa 11 mchana.katika kambi ya polisi wilayani bariadi.

Kamanda Chatanda amesema chanzo cha askari huyo kutenda tukio hilo ni kutokana na kutoridhishwa na maendeleo ya masomo ya mtoto huyo anayesoma shule binafsi ya gapa mjini bariadi.

0/Post a Comment/Comments