Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amewahakikishia Wafanyabiashara na
wawekezaji kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuweka
mazingira Bora ya biashara pamoja na kutatua changamoto za Wafanyabiashara.
RC
Makalla amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Biashara
Mkoani humo lenye lengo la kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara na kuweka
mikakati ya endelevu ya utatuzi wa changamoto za kibiasha zitakazowasilishwa.
Katika
kikao hicho RC Makalla amewashukuru Wafanyabiashara na wawekezaji kwa kuvunja
rekodi ya makusanyo makubwa ya Kodi Halali ambapo zaidi ya shilingi trilioni 10
zilikusanywa na TRA kwenye Mkoa huo.
RC Makala
amesema kuwa serikali itaendelea kuwa karibu na wafanyabiashara katika
kutengeneza Mazingira mazuri ya kufanya biashara zao.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara Tanzania Dkt. Godwill Wanga ameupongeza Mkoa wa Dar es salaam kwa kuendelea kufanikisha ufanyikaji wa biashara katika mazingira bora.
Katika hatua nyingine RC Makalla amesema Serikali ya Mkoa huo ipo hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa one stop center ya Biashara itakayokwenda kumaliza tatizo la urasimu.
Post a Comment