SACP NG'ANZI AWAELEKEZA MAAFISA WAKAGUZI KUSIMAMIA VIZURI MATUMIZI YA BARABARA

...............................

Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Ramadhani Ng'anzi amewaelekeza maafisa wakaguzi na askari wa R&F wa Mkoa kuhakikisha wanasimamia vizuri matumizi ya Barabara kwa wasukuma mikokoteni Ili kuongeza Usalama wawapo barabarani.

Pia Kamanda Ng'anzi amewataka wasukuma mikokoteni Hao kutumia barabara inavyotakiwa na hasa waisukume nyakati za mchana ili waweze kuonekana vizuri.

Kamanda Ng"anzi ameeleza hayo majuma kadha yaliyopita ambapo amewakumbusha watumiaji wote wa barabara hususani wasukuma mikokoteni kufuata sheria, taratibu na kanuni zote za usalama barabarani Ili kuepusha ajali zinazopelekea vifo na majeruhi.

Baadhi ya mambo yaliyozungumzwa na Kamanda ili iwe dira na maelekezo sahihi kwa wasukuma mikokoteni ni pamoja na na kuwataka wahakikishe wanazingatia kikamilifu sheria na kanuni zote za usalama barabarani.

"Usibebe mzigo mzito zaidi ya uwezo wako na uwezo wa mkokoteni wako,usisukume mkokoteni baada ya machweo ya jua baada ya Giza kuingia"amesema Kamanda Ng'anzi

Pia amewataka kusukuma mkokoteni pembeni kabisa Upande wa kushoto wa barabara,kuweka viakisi mwanga katika mkokoteni Ili uweze kuonekana kwa urahisi.

 

0/Post a Comment/Comments