..........
Serikali
ya Tanzania imepokea msaada wa vifaa vya kujikinga na magonjwa ya mlipuko kwa
ajili ya watumishi wanaotoa huduma za
afya na wateja wanaowahudumia,kutoka serikali ya Uingereza.
Makabidhiano
ya vifaa hivyo yamefanyika Bohari ya Dawa (MSD) Keko Dar es Salaam,ambapo
Mganga Mkuu wa serikali Prof. Tumaini Nagu amepokea vifaa hivyo kwa niaba ya
serikali kutoka kwa Mkurugenzi wa Maendeleo wa ubalozi wa Uingereza nchini
Tanzania, Kemi Williams.
Akipokea
msaada huo Prof. Nagu ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa vifaa hivyo na
kueleza kuwa vifaa vya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ni muhimu ili kupunguza
hatari ya watoa huduma kuambukizwa wanapotekeleza majukumu yao.
Vifaa hivyo vitasambazwa na MSD kama Wizara ilivyoelekeza.




Post a Comment