THE DESK CHAIR FOUNDATION IMEZITAKA TAASISI ZINGINE KUTOA MISAADA KWA JAMII

 


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Richard Mrusha Mwanza

MWENYEKITI wa  Taasisi ya The Desk Chair Foundation Muhamad Meghjee amezitaka taasisi mbalimbali nchini kujitokeza kuisaidia serikali katika kuwahudumia wananchi hususani kwenye maeneo yenye uhitaji wa maji kuwachimbia visima virefu vya maji safi na salama ili kuondolea aza ya maji ambayo imeonekana kuwa tatizo kubwa katika baadhi ya maeneo hapa nchi  licha ya jitihada kubwa za serikali kuendelea kuboresha huduma za maji.

Wito huo umetolewa hivi karibuni Jijini  Mwanza na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya The Desk Chair Foundation Madhjee wakati akikabidhi kisima cha maji kwa wananchi wa mtaa wa Kagomu uliopo kata ya Mahina ,Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza ambapo amesema kuwa iko haja ya kuongeza kasi ya kuisaidia serikali kuchimba visima kama inavyofanya taasisi hiyo ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.

Amesema kuwa katika mtaa huo kwa mujibu wa wananchi kulikuwa na tatizo kubwa la maji la muda mrefu hivyo  walipeleka maombi ya mahitaji ya kuchimbiwa kisima ofisini kwao na wao kama taasisi hawakusita kusaidia kwasababu ndio zima yao kubwa kuona wananchi wanapata maji.

"Mfano mimi nimezaliwa hapa Mwanza katika wilaya Sengerema kulikuwa na shida kubwa ya maji hivyo sisi kama familia imetupelekea  kuunda taasisi ambayo imejikita kutoa misaada mbalimbali ikiwepo kuchimba visima virefu vya maji safi na salama kwa ajili ya wananchi katika maeneo yenye ukame wa upatikanaji wa maji.'amesema Maghjee

Leo tunafuraha kubwa kukabidhi mradi huu wa maji ambao umekamilika kwaniaba ya wananchi wote wa eneo hili la  Mahina ,naomba mpokee kisima hiki cha maji na mitambo kama pamp,Sola,Betteri,Tanki la kuhifadhia maji ,vifaa vya usafi  na stoo ya kuhifadhia vitendea kazi."Amesema  ,Maghjee

Pia amewaeleza wananchi hao kuwa mradi huo wote sasa ni mali ya serikali ya mtaa  na wahudumiwe wananchi wote bila kujali tofauti zao za kikabila ,dini,rangi, pamoja na jinsia "Tunashukuru sana viongozi wa ngazi zote wa eneo hili na wananchi wote na mafundi wote waliohusika kwenye mradi huu ambapo leo wamefanikisha kukamilika kwa mradi kwa wakati muafaka na tayari wananchi wote wanapata huduma ya maji."amesisitiza

Maghjee amefafanua kuwa wao kama taasisi wataendelea kuchimba visima vingine vinne kwenye maeneo tofauti ili kupunguza msongamano kwenye kisima hicho cha kwanza huku akitoa rai kwa wananchi hao kukitunza na kukilinda na wao kama taasisi wasingependa kuona panajitokeza migogoro na ikabainika kuwa panamigogoro watakuwa wamewafukuza kabisa kwani wao sio waumini wa migogoro.

Na Kwaupande wake Mwenyekiti wa mtaa huo  George Peche amesema kuwa wamepokea mradi huo kwa mikono miwili na wamehaidi kuuulinda kwa hali na mali na wameshaweka utaratibu wa kulinda mradi huo ambao ni mkubwa katika eneo lao.

Amesema kuwa moja ya utaratibu ambao wameuweka ni wananchi wenyewe kuhakikisha wanakuwa walinzi wa mradi huo sambamba na hilo lakini pia wameweka walinzi wanne ambao watakuwa wanalinda kwa zamu na katika huduma hiyo ya  maji wananchi watakuwa wanachangia shilingi mitano kwa wiki ili kuwezesha kuwalipa walinzi hao ambao watakuwa na jukumu kubwa la kulinda mitambo kwenye kisima hicho.

mwisho.

0/Post a Comment/Comments