KAMPENI TOKOMEZA DAMPO BUBU KUZINDULIWA DAR ES SALAAM


Mratibu wa zoezia  la TOKOMEZA DAMPO BUBU DAR ES SALAAM akizungumza katika kituo cha Radio ya TBC Taifa kwenye kipindi cha MILINDIMO YA ASUBUHI

........................................

Na Mwandishi Wetu Dar Es Salaam 

KATIKA kuunga mkono jitihada za mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Amosi Makala kwenye zoezi la usafi la SAFISHA, PENDEZESHA JIJI Taasisi ya Orbit Environmental Consultancy imekuja kivingine na TOKOMEZA DAMPO BUBU DAR ES SALAAM ambapo kutakuwa na shughuli za usafi na kupanda miti katika maeneo yote yenye madampo yasiyo rasmi ili kuzuia uharibifu uliopo katika maeneo hayo na kusababisha athari kwa jamii hasa watoto

Mratibu wa zoezi hilo Moses Mwakibolwa hayo Jijini Dar Es Salaam wakati akiongea na kituo cha Radio ya TBC Taifa kwenye kipindi cha MILINDIMO YA ASUBUHI ambapo amesema zoezi la usafi na Upandaji wa miti  katika Jiji la Dar Es Salaam si kwa ajili ya kuhifadhi mazingira tu bali ni fursa ya kiuchumi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,  ambapo ametoa mfano wa tafiti za kimazingira zimeonesha kuwa  mti mmoja uliokomaa unaweza kunyonya hadi kiasi cha kilo 150 za gesi ya hewa ya ukaa kwa mwaka, lakini pia husaidia kupunguza joto, kusaidia kuboresha afya zetu za mwili na akili

Mwakibolwa ametaja baadhi ya fursa ambazo kama zikitumika ipasavyo  zitazalisha ajira kwa vijana na Jamii kupitia sekta hiyo muhimu, ametaja baadhi ya fursa ni taka za majumbani ikiwa ni pamoja na mifupa ya samaki, kuku ambavyo hutumika kama vyakula vya mifugo au mbolea asilia

“Ni dhahiri, kampeni hii ya usafi wa Jiji la Dar Es Salaam itakuwa na faida kubwa mbili, moja ni kuongeza kivutio kwa wageni wanaokuja Jjijini kila siku, lakini jambo la pili ni kasi ya upandaji miti unaofanyika hivi sasa, ambapo kutasaidia kutengeneza vivuli lakini pia sehemu ya kuchezea watoto baada ya sehemu nyingi kutotengwa maeneo ya watoto”

Mwakibolwa amesema zoezi hilo la usafi na kampeni ya TOKOMEZA DAMPO BUBU itaendelea kila ikiwa ni pamoja na Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya na itakuwa kampeni ya kudumu  ambapo amezitaka Taasisi zingine zinazojihusisha na mazingira kushirikiana naye na si kusubiri wanapokuja viongozi wakubwa na badala yake iwe tabia, ametoa wito kwa mashule, vyuo, taasisi na familia kuanzisha bustani ndogo  za miti zitakayomudu mazingira husika,

Mwakibolwa  ametoa wito kwa baadhi ya Taasisi zinazokata miti kwa ajili ya kuweka miradi hususani ya ujenzi, watenge fedha na maeneo mbadala kwa ajili ya kupanda miti au  kupunguza ukataji wa miti kiholela na kushauri uwepo wa sheria, kanuni na taratibu kabla ya kukata miti na kusema tupande miti kabla ya kukata mti

Mwakibolwa  alimalizia kwa kutoa shukrani kwa Shirika la habari Tanzania TBC pamoja na na vyombo vingine vya habari nchini, ikiwa ni pamoja na Radio, magazei na mitandao ya kijamii kwa kuhabarisha umma kuhusu athari na mabadiliko ya tabia nchi na  kujitoa kwao kuhakikisha kampeni hii inatekelezwa

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Tanzania Forest Services (TFS) kwa kujitolea na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hili kwa kutoa miti ya kutosha karibu kila eneo lenye miti basi kuna mkono wa (TFS)” alimaliza

0/Post a Comment/Comments